WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday 27 July 2013

ZFA wako wapi makocha hawa na zipi kazi zao wanazofanya?

Salum Vuai, Zanzibar

SITAKOSEA kama nitasema kwamba, miongoni mwa kazi za Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), ni kusimamia timu zetu za taifa, za wachezaji wa umri mbalimbali.


Kabla ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Rais wa ZFA Ali Ferej Tamim, uongozi wa chama hicho uliwahi kuwaita waandishi wa habari na kuwapa taarifa za utekelezaji wa mipango ya chama katika kuendeleza mpira wa miguu nchini.
Miongoni mwa mipango hiyo, ilikuwa kujenga timu imara za taifa kwa umri tafauti, kuanzia ngazi ya watoto na wakubwa.
Kupitia mkutano huo na waandishi uliofanyika mwaka 2011 katika ofisi za zamani za chama hicho zilizokuweko hoteli ya Bwawani, tuliambiwa na viongozi wa ZFA kuwa, imeamua kuteua makocha 14 kwa ajili ya kuchagua wachezaji na kuwafundisha katika timu mbalimbali za taifa.

Kwa upande wa timu ya wakubwa yaani Zanzibar Heroes, waliopewa jukumu la kuifundisha walikuwa, Stewart John Hall, na wasaidizi wake, Hemed Suleiman ‘Moroko’ na Ali Mohammed ‘Kidy’.Pia tukaelezwa kutakuwa na timu ya vijana walio chini ya miaka 23 (U-23).Hii ingefudishwa na Abdelfatah Abbas, raia wa Misri, akisaidiwa na Juma Sheha.
Aidha, Juma Sumbu alipewa jukumu la kuinoa timu ya vijana walio chini ya miaka 20 (U-20), na msaidizi wake, ni Ali Abdalla, wakati Mussa Jaribu akavishwa kofia ya kuifundisha timu ya wachezaji walio chini ya miaka 17 (U-17) sambamba na msaidizi wake Sheha Khamis.
Mbali na hizo, pia ZFA ilisema imeamua kuunda timu ya watoto walio chini ya miaka 15 (U-15), ambayo kocha wake ni Alley Mohammed Alley, huku Iddi Mohammed akitajwa kuwa msaidizi wa kikosi hicho.

Timu nyengine ni ile ya watoto wadogo wenye umri wa chini ya miaka 12 (U-12), ambayo kocha wake tulielezwa kuwa ni Hababuu Ali Omar, na Bundala Ramadhan, ndiye msaidizi wake.Na mwisho, ni timu ya taifa ya wanawake, ambayo kocha mwenye dhamana wa kuifundisha ni Nasra Juma Mohammed na msaidizi wake ni Ali Mohammed ‘Kidy’ ambaye pia ametajwa kuwa msaidizi wa Zanzibar Heroes.

Lakini jambo la kushangaza, tangu wakati huo, hakuna chochote kinachofanyika kuhusiana na timu hizo na namna ya kuziendeleza, yaani hazikuchaguliwa kabisa na inaonekana uteuzi wa makocha hao ulikuwa ni porojo za ‘kufurahisha barza’ tu.
Katika hali ya kawaida, baada ya ZFA kuteua makocha hao, ilipaswa iwape taarifa za maandishi juu ya uteuzi wao, na ifanye nao kikao ili kuwafafanulia majukumu yao.
Yawezekana hayo yalifanyika, lakini ni kwa kiasi gani makocha hao waliwezeshwa kufanya ziara katika wilaya zote Unguja na Pemba ili kuangalia mashindano mbalimbali na kuchagua wachezaji wa kufaa kuzichezea timu hizo.

Nina hakika hakuna jitihada zozote zilizochukuliwa kuhakikisha makocha hao wanafanya kazi waliyopewa, kwa kuwa ZFA yenyewe haina chanzo chochote cha kupata fedha za kutekeleza shughuli zake, sikwambii kusimamia timu saba za taifa.
Ni rahisi kusema kwa mdomo kwamba mtu au taasisi inakusudia kufanya hili au lile, lakini unapofika wakati wa vitendo, kama hakuna fedha, hakutafanyika kitu, na ndivyo ilivyotokea.Kubwa tunalolishuhudia, ni kushughulikiwa kwa timu ya wakubwa, Zanzibar Heroes, tena hilo hufanyika kila wakati wa mashindano ya Chalenji yanayoshirikisha timu za mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.

Na hili nalo kwa kiasi kikubwa linabebwa na serikali, au pale wanapotokea wadhamini, huchangia walichonacho kugharamia mahitaji ya timu ikiwemo kuipatia vifaa wa ajili ya mashindano.Mimi huwa ninajiuliza, huwaje chama kikubwa kama ZFA kifanye maamuzi ya kukurupuka, na kushindwa kujiendesha kisasa?Ni wazi kuwa ZFA inakosa wataalamu ambao ingeweza kuwatumia kupanga mpango kazi wake na kuusimamia ipasavyo.
Lakini hata ikiwa nao watu walio weledi, itawezaje kuwalipa ikiwa yenyewe ina mzigo wa madeni, hasa lile la kodi inayodaiwa na hoteli ya Bwawani ambayo imefikia shilingi milioni 14 sasa? Kwa hivyo, kama haina uwezo huo, kwa nini iwaite waandishi wa kujikweza kwamba ina mipango mingi na mizuri lakini mwisho wa habari ishindwe kuitekeleza? Tukiacha timu za umri mwengine, ZFA inaweza kueleza, kwa nini inashindwa kumtumia ipasavyo kocha Abdelfatah Abbas ambaye serikali ya Misri ilimleta msaada kwa ajili ya maendeleo ya soka zanzibar.
..........
HAPO NYUMA KUPITIA KATIKA BLOG HII YA KITUO CHA KUKUZA VIPAJI VYA SOKA KWA VIJANA KULIWAHI KUTOLEWA MAONI YA SUALA LA MAENDELEO YA SOKA KWA VIJANA JINSI YA KUTOKUWEPO KUSHIRIKIANA KATI YA WIZARA YA UTALII NA WIZARA YA MICHEZO AMBAZO ZOTE NI WIZARA MOJA.

KAMA KUTAKUWA NA UTARATIBU KWA KILA MTALII ANAEINGIA NCHINI AIDHA KUPATA DOLA MOJA AU NUSU DOLA ANAPOINGIA AU KUTOKA NCHINI AU KUPITIA KATIKA NYUMBA ZA KULALIA WAGENI AU SEHEMU YOYOTE ILE FEDHA HIZI NI KWAAJILI YA KUIBUA NA KUKUZA SOKA KWA UPANDE WA VIJANA BASI HILO NI SUALA AMBALO SIO KUBWA KULIKO KUSUBIRI KUTEGEMEA KUSUBIRI WAFADHILI.

SOKA NI AJIRA KWA VIJANA WENGI HIVYO SERIKALI IKIWEKEZA ITAWEZA KUJIPATIA FAIDA KWA KUTOA AJIRA KWA VIJANA WAKE AMBAO WENGI WAO WANAKUWA NI VIGUMU KUPATA KAZI ZA OFISINI AU SEHEMU NJINGINE NA KUPELEKEWA WIMBI LA VIJANA KUKOSA KAZI .

MBALI NI HILO SOKA NI MCHEZO UNAOPENDWA NA WATU WENGI NCHI YOYOTE ILE DUNIANI HIVYO KAMA SERIKALI YOYOTE DUNIANI INATAKIWA IHESHIMU PIA WANANCHI WAKE NA MAPENZI YAO KWANI SIO KILA MTU MWANASIASA.

SERIKALI KIKAWAIDA INASHINDWA KUWAUNGANISHA WANANCHI WAO KATIKA SIASA LAKINI WANANCHI HAO HUUNGANA NA KUWA  WAMOJA KATIKA MAPENZI YA TIMU ZAO ZA SOKA HIVYO HIO PIA NI FARAJA KWA NCHI WANANCHI KUWA PAMOJA.

HATA HIVYO TUNATARAJIA HARAKA SANA KUONA TIMU ZA TAIFA KUANDIA U12 HADI TIMU YA WAKUBWA ZINAREJEA KUANZA KAZI KAMA MIPANGO ILIVYOWEKWA HUKO NYUMA, TUNATARAJIA BADO ZFA INA NIA NA MPANGO HUU AMBAO LABDA TU BADO UPO OFISINI KATIKA MAKARATASI NA SASA NI MUDA WAKE MZURI WA KUUFANYIA VITENDO KWA MAENDELEO YA TAIFA.