WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Friday 10 July 2015

MATAYARISHO YA U17 KUELEKEA 2017




        (Vijana pichani  wakiwa kazini katika uwanja wa Amaan katika mechi za ligi zao 2014/2015)

Chama Cha Soka cha Vijana Wilaya ya Mjini (Kamati ya Central Leugue) kinawaomba wadau wao kuwatupia macho vijana hawa ambao ndio Taifa la kesho hasa,ukizingatia hivi sasa Tanzania inakabiliwa na mashindano magumu ya soka kama mwenyeji wa U17 kwa nchi za Afrika hivyo huu ni wakati muwafaka kwa vijana hawa kulisaidi Taifa letu katika umri huu,

Kama inavyojulikana Wilaya ya mjini imetoa nyota kadhaa wa soka wa Taifa kupitia katika utamaduni huu wa soka ya vijana kwa zaidi ya miaka 50 kuwa na ligi za vijana wa umri mbalimbali,hivyo hii ni fursa kubwa kwetu kuweza kuonyesha uwezo wa kusaidiana na timu za vijana pamoja na Chama hichi cha soka kwa Vijana ili tuweze kufikia malengo kwa manufaa ya Taifa letu.

Ni mara kadhaa ubora wa vipaji wa vijana wa wilaya mjini umeonekanwa kwa kutwaa ubingwa wa Copa Coca Cola huku ikizifunga timu za mikoa yote ya Tanzania hivyo hii ni fursa kwa wandinga chipukizi wa wilaya hii kuweza kulikomboa Taifa letu hasa katika mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya vijana wa umri huo katika bara la Afrika na bila shaka Zanzibar itakuwa ni moja ya kituo cha mashindano hayo.

Tunaomba wadau wote kwaniaba ya Taifa letu kuwasaidia vijana hawa ili kuhakikisha wanapata nafasi tosha katika timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17 miaka miwili ijayo kuanzia sasa,itakuwa ni jambo la aibu kuona wilaya yetu ya mjini wilaya yenye vipaji vya vijana katika ligi zetu zaidi ya miaka 50 sasa kukosekana hata wachezaji vijana wa maana watakaokuwa na uwezo wa kuitwa katika timu ya Taifa ya Tanzania U17 mwaka 2017.

Hii ni fursa tosha kwa wadau wa wilaya ya mjini wa ndani na nje kuwasaidia vijana wetu kulitangaza Taifa letu hasa ukuchukulia maanani mashindano hayo yatakuwa yakifuatiliwa na mawakala,makocha,na viongozi wa vilabu karibu vyote vikubwa na vidogo vya barani ulaya kusaka vipaji kwaajili ya vilabu vyao,hivi sasa vilabu vingi vya barani ulaya vimeamka na kuwekeza zaidi katika kusaka vijana wenye uwezo wa kusakata soka na safari hii itakuwa tupo nyumbani,katika uwanja wa nyumbani,katika ardhi ya Tanzania hivyo ni fursa tosha na  kutowaachia nafasi hizo Ivory Coast,Cameroon,Nigeria na wengineo.


Timu ya Taifa ya Tanzania U15  inatarajiwa kuwasili Zanzibar mwezi ujao na kucheza na magwiji wa soka waliobobea katika fani ya soka ya umri huo, nadhani hii ni nafasi nzuri kwa wadau kushirikiana na vijana chipukizi ili kuweza kumuonyesha na kumshawishi kocha wa Timu hio ya Taifa ya Tanzania uwezo na kile ambacho kunafanywa na vijana hao katika mashindano ya soka yenye uzoefu wa zaidi ya miaka 50 iliyopita hivyo kutoa fursa kwa mwalimu huyo wa Taifa kuwaona na kutoa vijana wengi iwezekavyo katika timu yetu ya wilaya ya mjini ambao wataonekanwa pia katika Tv za mabara yote wakati wa mashindano hayo ya mwaka 2017.

Ndugu wadau hii ni nafasi ya kutoijutia kama kutakuwa na ushirikia wa pamoja kwa hali yoyote ile ambayo kila mdau atahisi inafaa katika mchango wake wa maendeleo haya kuelekea 2017 ambayo haiko mbali kuanzia leo.