WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Wednesday, 14 October 2015

RUNGU LA FIFA LAIBUKIA ZFA ZANZIBAR

ZFA 1

Na Abubakar Kisandu, Zanzibar
Baada ya jana Mahakama kuu Zanzibar kuamua  kutoa agizo la kuwataka viongozi wote wakuu wanaohusika na kesi nambari 62 ya mwaka 2014 kutojihusisha na shughuli zozote za ZFA, leo umoja wa vilabu Zanzibar wametangaza kamati ya mpito itakayosimamia shughulizi zote za mpira wa miguu kwa ngazi ya Taifa.

Akiwataja viongozi hao kwenye kamati hiyo ya mpito, Ali Ussi (Jongo) ambae ni katibu wa umoja wa vilabu amesema wao ndio waliopewa dhamana hiyo na mahakama kuunda kamati ya mpito.
Katika kamati hiyo iliyotangazwa leo ina jumla ya watu 7 ambapo mwenyekiti ni Hussein Ali Ahmada, mwenyekiti msaidizi atakuwa Omar Ahmed Awadh, katibu mkuu Hashim Salum Hashim, na katibu msaidizi Khamis Hamad.
Wajumbe kwenye kamati hiyo ni Ussi Ali Jongo, Massoud Attai, na Salum Hamdun.
Kamati hiyo inatarajiwa kukutana kwa mara ya kwanza siku ya Alhamis ya tarehe 15/10/2015 saa 4:30 asubuhi kwenye ukumbi wa uwanja wa Amaan ambapo wakitarajia kazi yao ya kwanza kufanya kikao cha usuluhishi na timu ya Chuoni ili waondoshe shauri lao mahakamani na kuruhusu mpira kuchezwa visiwani Zanzibar, kazi yao ya pili ni kufanya mazungumzo na timu ya Aluta ya Mwanga Pwani na wao waweze kuondosha shauri lao mahakamani ili pia ligi daraja la pili taifa ichezwe.

Aidha katibu Jongo amesema wao kama umoja wa vilabu wamepewa dhamana hiyo ya kuunda kamati na mahakama na mtu yoyote ambaye  hawaamini waende mahakamani wakaulize ambapo pia wakiwa na imani kuwa kamati hiyo isifike hata miezi 5 na viongozi hao wa muda kama watafanya kazi vizuri ndani ya kamati hiyo ya mpito basi  watawachagua kwenye uchaguzi wa chama hicho.

Baadhi ya Waandishi wa habari waliofika kwenye uteuzi huo wa kamati ya mpito waliuliza kwanini wajumbe ni wachache (7) wataweza kweli kuendesha shughuli hizo?
“Jamani hii ni kamati ya mpito ndio maana ni wachache, hakuna haja ya kuwepo rundo la wajumbe” alisema Jongo.

Kamati hiyo imeundwa leo baada ya jana Mahakama kuu ya Zanzibar kuuamua  kutoa agizo la kuwataka viongozi wote wakuu wale wanaohusika na kesi nambari 62 ya mwaka 2014 kutojihusisha na shughuli zozote za ZFA, viongozi ambao wanadaiwa na mdai yani aliyefungua mashtaka Haji Ameir (Mpakia) na waliofunguli wa kesi hiyo ambao ni rais wa chama hicho Ravia Idarus, Katib Kassim Haji Salum na Makamo rais ZFA Pemba Ali Mohammed wote kutakiwa na mahakama kutojihusisha na jambo lolote linalohusu ZFA mpaka kesi hiyo imalizike ambapo itaendelea tena tarehe 12 mwezi November.

chanzo-Shaffi Dauda.Na Ameir Khalid, ZANZIBAR

SIKU moja baada ya Mahakama Kuu ya Zanzibar kuwaamuru viongozi wa juu wa Chama cha Soka (ZFA) kuondoka madarakani, kamati ya muda kwa ajili ya kusimamia shughuli za chama hicho imeundwa.
Juzi, Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mkusa Isaac Sepetu, wakati akisikiliza kesi inayowakabili viongozi hao, Rais wa ZFA Ravia Idarous, Makamu wake ofisi ya Pemba Ali Mohammed pamoja na Katibu Mkuu Kassim Haji Salum, alisema kwa mujibu wa katiba ya ZFA muda wao wa kukaa madarakani umemalizika hivyo wakae pembeni.

Jaji Sepetu pia alitoa agizo la kuundwa kamati ya muda ya uongozi wa chama hicho ambacho mbali na kesi ya ubadhirifu wa fedha, inakabiliwa na kesi mbili za kukiuka katiba na kanuni za mashindano, zilizofunguliwa dhidi yake na klabu za Chuoni SC na Aluta.
Kufuatia amri hiyo ya mahakama, Umoja wa Klabu za Soka Zanzibar umetaja kamati ya watu saba ambayo itakuwa na jukumu la kuweka mambo sawa ili shughuli za mpira wa miguu ziendelee, pamoja na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa chama hicho kupata viongozi wapya.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa uwanja wa Amaan, Katibu wa umoja huo Ali Ussi Jongo, aliwataja walioteuliwa kuunda kamati hiyo kuwa ni Hussein Ali Ahmada anayekuwa Mwenyekiti ambapo Makamu wake atakuwa Omar Ahmed Awadh.
Aidha, Hashim Salum Hashim anakuwa Katibu Mkuu akisaidiwa na Khamis Hamad, wakati Masoud Attai Masoud, Salum Hamdun na Ali Ussi Jongo wanakuwa wajumbe wa kamati hiyo.
Jongo alisema miongoni mwa majukumu makubwa ya kamati hiyo ni kuzungumza na uongozi wa klabu za Chuoni SC na Aluta, kuziomba ziondoshe kesi walizoifungulia ZFA ili mpira uchezwe na ligi zianze.
Aidha, alisema kazi nyengine ni kuandaa utaratibu wa kufanya uchaguzi mkuu wa chama hicho ambacho kwa muda sasa shughuli zake zimekwama kutokana na kuelemewa na mzigo wa kesi mahakamani.

Akizungumza na gazeti hili baada ya kuteuliwa kwake, Mwenyekiti wa kamati hiyo Hussein Ali Ahmada (pichani) ambaye pia ni Katibu wa kituo cha kukuza vipaji cha Oranje (OFA), alisema kazi waliyopewa ni ngumu lakini anaamini wakipata ushirikiano wataifanya kwa ufanisi mkubwa. 
"Kwa kuwa nia yetu sote ni kuona soka linachezwa na kuendelea, na pia mimi nilikuwemo kwenye kamati ya usuluhishi kumaliza mzozo ndani ya ZFA, bila shaka kwa pamoja tutaweza kurejesha hali kuwa ya kawaida," alifafanua.
Taarifa zaidi zilizopatikana na gazeti hili, zimefahamisha kuwa, ifikapo Jumamosi, mambo yote yanayokwamisha shughuli za ZFA yatakuwa yamemalizwa na kubaki kuwa historia. 

Chanzo-Bin Zubeiry

Mahakama Kuu Zanzibar yauengua uongozi wa ZFA madarakani, Kamati ya muda yaundwa

Na Ameir Khalid, ZANZIBAR

Chanzo-Habari Leo