Kutokana na wanataaluma wa soka duniani kote wanasema " Timu yoyote isiyokuwa na timu zake za watoto basi sio timu, bali ni wababaishaji tu,katika ulimwengu wa kisasa wa maendeleo ya soka inatokana na vijana ambao emewajengea mazingira yako kitimu tokea katika umri mdogo"
Nadhani hili litaweza kuwapatia faida kubwa sana JKU miaka michache ijayo na kuokoa mamilioni ya fedha za usajili wa wachezaji wa kuja na kuondoka kutoka vilabu mbalimbali, pia mbali na kuwa na uhakika wa nyota wengi chipukizi watakaovuna kila mwaka kwaajili ya kuwatumia wenyewe katika mashindano mbalimbali bali pia wataweza kuwauza wachezaji wao ndani na nje ya nchi bila klabu yako kutetereka kutokana na kuwa na " kisima" cha wachezaji vijana wanotokana na mpango wao huo endelevu waliouanzisha hivi sasa.
Kituo chetu cha kukuza soka kwa vijana cha O.F.A kinatoa pongezi kwa mara nyingine kwa uongozi wa JKU na pia kutoa ushauri kwa vilabu vyote vya madaraja ya juu kufata mfumu huu wa kisasa katika kukuza soka nchini,kwani mbali ya vilabu kunufaika na wachezaji hao vijana kila mwaka pia kutawafanya wachezaji hao chipukizi kuzidi kujituma kwa bidii kwani watakuwa na uhakika kwa jitihada zao wataweza kupata nafasi za kwenda moja kwa moja katika timu kubwa zinazoshirikiana nazo.
Nadhani kuna baadhi ya vilabu vinaona ni gharama kuwa na vilabu vya watoto wakati ni gharama zaidi kutokuwa na vilabu vya watoto kwani miaka itakwenda na vilabu hivyo vitakuwa vikipoteza muda bila mafanikio yoyote kutokana na kutojijengea misingi mizuri kama ambavyo JKU wameamua kwa makusudi kabisa baada ya kuona nini itakuwa faida yake hapo baadae.
Kuna Vilabu vingi vya vijana nchini ambavyo pia vinaweza kushirikina na vilabu vikubwa kuwa kama mashamba yao ya wachezaji kama kutakuwa na mikataba mizuri itakayoandaliwa kushirikiana na vilabu hivyo vya vijana, huu ni muda muwafaka kwa uongozi wa ZFA Taifa kuvilazimisha vilabu vyote vya madaraja ya kwanza,pili na Tatu kuwa na vilabu vidogo vinavoshirikiana navyo ili msimu ujao kuwe na ushindani wa michuano ya soka ya vilabu vidogo vinavyoshirikiana na vilabu vikubwa hivyo itatoa fursa kwa viongozi wa vilabu vyao vikubwa kushiriki kuangalia ni jinsi gani vijana wao wanaimarika kupitia mashindano hayo ambayo yatakuwa ni maendeleo ya Taifa letu miaka ya baadae.
Watoto chini yav Umri wa miaka 14 wakiwa katika zoezi la uchaguzi wa Timu ya Watoto inaoyundwa na Timu ya JKU Academy Zanzibar. wakiwa katika jukwaa la uwanja wa amaan Zanzibar.
Wachezaji wa Timu za Watoto chini ya Umri wa miaka 15 wakiwa katika zoezi la mchujo wa Vijana 60 watakaounda timu ya JKU Acedamy, kukuza Vipaji vya Wachezaji Zanzibar na kuweka kambi yao katika Kambi ya JKU Saateni.
Watoto chini ya Umri wa miaka 15 wakiwa katika mazoezi ya mchujo wa Timu ya Watoto wa Chuo cha JKU cha Academy Zanzibar. kukuza vipaji vya wachezaji Zanzibar kupitia Chuo hicho.
Meneja wa Timu ya JKU Zanzibar akifuatilia mazoezi hayo ya Mchujo kwa Watoto watakaounda timu ya Watoto wa Umri wa miaka 15 ya JKU Acedamy.
Jopo la Makocha wa Vikosi vya SMZ Zanzibar wakiwa katika zoezi la kuchagua Vijana wenye vipaji kuunda Timu ya Watoto wa Chuo cha JKU Acedamy yenye umri wa miaka 15. wakiwa katika jukwaa la uwanja wa amaan wakati wa zoezi hilo likifanyika kwa watoto mbalimbali waliojitokeza katika mchujo huo.
Mwalimu wa chipukizi wa Academy akiwaelekeza chipukizi wake wakati wa mazoezi hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Amaan.Habari hizi ni kwa hisani ya Zanzinews.