WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday 27 June 2009

MAZOEZI ORANJE FOOTBALL ACADEMY YASIMAMA KWA MUDA MFUPI

Mazoezi ya vijana wa Oranje Football Academy yamesimamishwa kwa muda mfupi kutokana na kuwapa nafasi chipukizi wa O.F.A kupata mapumziko kidogo,kutokana na kutotangazwa kwa tarehe ya mechi ya Final ya knock-out viongozi wa O.F.A kwapamoja wameamua kuwapatia vijana wao mapumziko ya muda mfupi hadi hapo watakapowatangazia kuanza mazoezi muda mfupi ujao,

akitangaza kuhusu kusimamishwa mazoezi ya vijana hao ambao wanasifika kwa kusakata soka ya kisasa wakiwa uwanjani katibu mkuu wa O.F.A Ali Hussein (pichani)aliiambie blog hii inayomilikiwa na O.F.A kuwa baada ya kukutana viongozi wote na kutathmini ligi na wachezaji wameamua kuwapumzisha vijana hao kwa muda ili kuweza kuwapa nafasi ya mapumziko kidogo na kuweza kurejea kiwanjani na nguvu mpya watakapoanza tena mazoezi hivi karibuni,

katika yaliyozungumziwa katibu mkuu Hussein alisema wapo katika hatua ya pili ya kuimarisha Academy ya O.F.A
ambapo itaweza kuwawacha baadhi ya wachezaji viwango vyao vilivyoshuka kisoka na kuongeza nguvu mpya aidha kuwawacha wale ambao walioonyesha upungufu wa nidhamu kwa muda wote waliokuwa na O.F.A,

lengo ni kuweza kupata academy imara ambayo itakuwa na uwezo wa hali ya juu kisoka,pamoja na nidhamu,wachezaji vijana wanahitajia sio tu kuwa na vipaji vya soka bali nidhamu ni msingi wa maendeleo kwa kila mchezaji hasa vijana kwani huwapelekea kuzoea hadi watakapofikia kisoka,
katika mwaka wake wa kwanza O.F.A walifanikiwa kushika nafasi ya 3 katika ligi ya youth U-17,na kuonyesha kiwango cha hali ya juu kisoka,pia walitwaa bonanza cup iliyodhaminiwa kwa ushirikiano wa makampuni za Zanzibar Explore na ZanAir,na hivi sasa O.F.A wapo na mchezo wa Fainal ya knock-out,

katibu mkuu alisema ni matokeo mazuri sana kwa vijana wake ambapo ni mwaka mmoja tu sasa kuweza kuwa pamoja, "tunaamini msimu unaofata tutaweza kuwa na timu imara mara mbili ya hii ya sasa kwani vijana wetu wamekuwa wakizoweana kimchezo kila siku pamoja na wachezaji wapya ambao tutaweza kuwaongeza kwa msimu ujao tunaamini tutakuwa na academy imara sana"-aliongeza katibu mkuu wa O.F.A ,

hivi sasa O.F.A wapo katika kuangalia kuongeza wachezaji wapya ambao walikuwa wakiwafatilia tokea kuanza kwa ligi ya Youth U-17 hadi kumalizika, tayari kuna majina ya wachezaji ambao wameonyesha vipaji vya hali ya juu katika timu zao na wamekuwa ni nyota kuanzia mwanzo wa ligi hadi mwisho ambapo makocha wa O.F.A wamewaona kuwa wanafiti sana katika academy ya O.F.A ambapo wataweza kuziba mapengo ya wachezaji ambao watawachwa kutokana na kupungua viwango,pamoja na upungufu wa nidhamu ambao hawana sifa za kubakia katika academy ya O.F.A,

katika mikakati ya O.F.A ni kuitangaza Tanzania katika soka nje ya nchi ambao chipukizi hao wataweza kuiwakilisha Tanzania katika MILK CUP YOUTH TOURNAMENT ambayo itafanyika katika mji wa BELFAST-NOTHERN IRELAND ambapo michuano hiyo hufanyika kila mwaka na hushirikisha timu za youth kutoka nchi mbali za Euroeper na South America,

hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa timu ya youth kutoka bara la Africa kushiriki katika mashindano hayo barani ulaya ambapo huhudhuriwa na makocha mbali mbali wa vilabu vikubwa vya ulaya pamoja na scouting agents ambao huwakilisha vilabu kusaka vipaji kwaajili ya timu wanazoshirikiana nazo kupeleka wachezaji vijana, hii itakuwa ni nafasi kubwa kwa O.F.A kuiwakisha vizuri Tanzania na kuitangaza kisoka,

mipango inaendelea kufanywa ya ushiriki wa O.F.A katika michuano hio ambapo viongozi wao waliopo Belfast-Nothern Ireland wapo katika hatua nzuri tahehe pamoja na mwezi itatangazwa mara baada ya kukamilika kila kitu.

Oranje football Academy ina walimu imara ambao wameweza kutoa wachezaji mbali mbali nchini akiwemo Coach Hassan ambae ndio mwalimu aliewapandisha viwango wachezaji Nadir Haroub "Canavaro" pamoja na Abdi Kassim "Babi", pamoja na wachezaji wengi ambao wanachezea vilabu mbali mbali vikubwa nchini pamoja na nje kama vile Nassor Ali "Kibichwa" anaechezea NewCastel United Academy ya England,Adam Nditi anaechezea Chelsea Academy ya England pamoja na sleiman Leluu anaechezea coventry City U18 pamoja na England National Team
U-18,
tunatarajia katika academy yetu ya O.F.A kutoa nyota wengi siku za hivi karibuni na tunatarajia kila ambae atahitajia kutoa msaada/mchango wake kwa vijana wetu tunamkaribisha, tunataajia hivi karibuni pia kuwatangaza Mwenyekiti pamoja na katibu mkuu msaidizi wa academy yetu.
-------------------------------------------------------------------------------------------------