WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday, 4 July 2009

ORANJE FOOTBALL ACADEMY YATWAA TAJI JINGINE LA YOUTH KNOCK-OUT U17

Mabingwa wapya wa Knock-out 2009 kwa timu za youth U-17 wamepatikana dakika chache zilizopita,Oranje Football Academy vijana wenye kusakata soka la kisasa wameweza kutwaa ubingwa leo katika kiwanja cha mao tse tung kwa kuichapa timu ya vijana ya F.C Arizona kwa jumla ya mabao 2-1,

katika mchezo safi ambao ulimalizika dakika chache zilizopita mechi ambao ilikuwa kali na upinzani mkubwa kwa pande zote mbili,

katika mechi hio ya leo ya Fainal mabao ya vijana machachari wa O.F.A yalifungwa moja kwa kila kipindi, bao la kwanza lilifungwa na mshambulia hatari Said Mbaroud(malouda)

na lile la ushindi lilipachikwa wavuni na Yahya Mudathir katika kipindi cha pili,

kwa ushindi wa leo O.F.A itakuwa imetwaa mataji mawili msimu huu 2009 baada ya kutwaa ubingwa wa Bonanza Cup mwanzo mwa mwaka huu,
katika mechi ya leo O.F.A wamewakosa washambuliaji wao wawili Seif Abdalla(kahire) pamoja na Ali Hilali(Lee) ambao wapo katika mashindano ya Coca Cola Cup yanayondelea jijini Dar es Salaam,
pamoja na wachezaji hao imewakosa wachezaji wake kadhaa ambao wanasumbuliwa na maumivu mbali mbali waliyoyapata wakati wa mazoezi kujiandaa na mechi hio ya leo,
pamoja na kuwapoteza wachezaji hao muhimu vijana hao wa O.F.A wamekuwa na hazina kubwa ya chipukizi wenye vipaji vikubwa na ndio iliyopelekea leo kuweza kuendeleza kutembeza kichapo kwa kila timu wanayokutana nayo na kutwaa ubingwa kwa mara nyingine kwa mwaka huu 2009,
picha na maelezo zaidi kupatikana baadae katika blog hii inayomilikiwa na chipukizi hao wa Oranje Football Academy.