WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Friday 7 August 2009

MUDATHIR KINDA MWENYE UWEZO NA KIPAJI KIKUBWA KISOKA

Kinda wa O.F.A Mudathir Abbas akipokea kikombe kama zawadi ya mchezaji bora wa mashindano ya knock-out mwaka huu 2009.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Mchezaji chipukizi Mudathir Abbas akiwa na zawadi ya uchezaji bora mwaka huu 2009
-------------------------------------------------------------------------------------------------
JINA : MUDATHIR YAHYA
KAZI : MWANAFUNZI/SOKA
UMRI : 14 YRS
TAREHE YA KUZALIWA : 13th OKTOBER 1995
NAFASI YA UCHEZAJI : KIUNGO MSHAMBULIAJI
MGUU : KULIA NA KUSHOTO
UREFU : 1.66 CM
UZITO : 58 KG
Mudathir Yahya Abbas mchezaji chipukizi mwenye uwezo wa hali ya juu na kipaji cha aina yake katika kusakata soka,
akiwa na umri wa miaka 14 tu Mudathir amethibitisha kuwa ni mmoja ya mchezaji mwenye kipaji kikubwa zaidi kuliko umri wake ulivyo,
ni mchezaji anaetulia sana akiwa uwanjani na hufanya vitendo ambavyo havitarajiwi na yeyote ambae atakuwa akimuangalia akiwa uwanjani,
Chipukizi huyo ambae anachezea katika nafasi ya kiungo mshambuliaji ni muunganishaji wa timu yake ya O.F.A kati ya ulinzi,katikati na ushambuliaji,ni kijana ambae kutokana na staili zake huwapoza wachezaji wenzake kuwa na utulivu kiwanjani pamoja na kupangilia mchezo wote ambao unawakabili,
Oranje Football Academy inafarijika sana kwa uwezo wa Kinda huyo kwa uwezo wake mkubwa wa kuwa kama ni mchezaji wa mwisho kuunganisha pasi za kumalizia kupachika mabao vilevile akiwa ni kama ni mfungaji pia wa O.F.A
Katika ligi ya U-17 ambayo ina jumla ya michezo 17 kuanzia ngazi ya makundi hadi katika vilabu 9 bora vya vijana vilivyoshinda katika makundi yao Mudathiri aliweza kuvaa jezi ya Oranje Football Academy mara 16 ambapo kati ya mechi hizo aliweza kupachika mabao 8 kimiani akiwa kama kiungo na kusababisha kadhaa ambapo O.F.A walimalizia ligi hio wakishika nafasi ya 3.
Uwezo wa hali ya juu ulioonyeshwa na kijana Mudathir ulizidi kudhihirika pale alipoweza kuwa nyota katika kila mechi ambayo alicheza katika mashindano ya knock-out U-17 ambapo alitoa mchango mkubwa na pia kuwa kichocheo cha O.F.A kutwaa ubingwa huo.
Robo fainali ya mashindano hayo kijana huyo chipukizi alifanya kama kawaida yake katika mchezo waliocheza na wapinzani wao Shangani f.c ambapo matokeo yalikuwa ni 2-1 huku mabao yote mawili yakipachikwa wavuni na Mudathir kwa upande wa O.F.A .
kwenye mechi ya Nusu Fainali O.F.A v/s F.C Kipago kijana huyo alizidi kungára kwa kucheza mchezo maridadi katika nafasi ya kiungo pamoja na yeye mwenyewe akisukuma na kuongeza mashambulizi ambapo matokeo yalikuwa O.F.A ilishinda 1-0 bao lilipachikwa wavuni na Mudathir Abbas.
Kama hio haitoshi Kinda huyo aliweza kutawala katika nafasi ya kiungo katika mechi ya fainal ambayo aliwadhihirishia viongozi,wachezaji wenzake,mashabiki na wapenzi wa soka waliofurika kuona mechi ya fainal na kuiongozi O.F.A kutwaa ubingwa kwa kutengeneza pasi maridadi ambayo ilimkuta mfungaji wa bao la kwanza,
katika dakika za majeruhi kijana Mudathir alikamilisha kazi yake ya kuonyesha kuwa mbali na kuwa umri wake ni mdogo lakini uwezo wake ni mkubwa sana katika soka pale alipopachika bao la ushindi na lililopekea ubingwa kwa vijana wa Oranje football Academy,ambapo mbali ya kuchaguliwa Man of the Match wa Fainali hio bali pia alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo ya knock-out
Mudathir Abbas ni nyote ambae bila shaka taifa litajivunia hapo baadae ambapo ndoto yake ni siku moja kucheza soka ya kulipwa nje.
-------------------------------------------------------------------------------------------------