WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Thursday 3 September 2009

MDUTCH WA ORANJE FOOTBALL ACADEMY ATUA NCHINI

Kiongozi wa Oranje Football Academy ISABEL DEN HEIJER ambae ni mwandishi na mpangaji shughuli mbalimbali za kituo cha kukuza soka kwa vijana cha O.F.C amewasili nchini juzi tayari kuanza shughuli zake kwa vijana hao wa O.F.A.

Den Heijer (pichani)ambae ni raia wa Holland aliwasili jijini Dar Es Salaam juzi akitokea Kenya ambapo alikuwa kazini katika mambo ya watoto ambapo alitembelea na kutoa huduma mbalimbali kwa watoto wa vijiji kadharaa vya nchini humo.

Kiongozi huyo kutoka Holland ni mmoja wa viongozi kadhaa wa kigeni wa kituo hicho cha kukuza vipaji vya watoto nchini ambapo mbali na Holland O.F.A ina viongozi nchi kadhaa katika bara la Ulaya ambapo wanatarajia kutoa misaada kwa kuwapatia vijana wake kwenda kucheza soka ya Kulipwa siku zijazo.

Den Heijer atakwenda Zanzibar na ataweza kutambulishwa rasmi kwa viongozi na wachezaji wa O.F.A siku ya tarehe 27 ya mwezi wa Ramadhani.

Mbali na Den Heijer Oranje Football Academy itaweza kutambulishwa Vice President wake ambae ni MTanzania anayeishi nchini Nothern Ireland ambae atawasili nchini wiki ijayo.

Pia katika ghafla hio fupi iliyoandaliwa na O.F.A kutakuwa na utambulisho wa kiongozi mwengine ambae amechaguliwa kuwa Mwenyekiti na msemaji mkuu wa O.F.A ambae pia anamadaraka katika ngazi kuu ya soka Tanzania.

baada ya Utambulisho huo Isabel Den Heijer ataweza kukabidhi vifaa vya soka kwa vijana hao O.F.A ambao ni mchango wake binafsi kutoka Holland ambapo vifaa hivyo vitaweza kuwasaidia vijana hao kisoka.

akiongea na Web Blog ya O.F.A katibu mkuu wa O.f.A Hussein amesema baada ya sherehe hio fupi ya kutambulishana viongozi,kukabidhiana vifaa pamoja na kubadilishana mawazo kidogo yatakayofanyika mchana katika siku ya 27 ya mwezi wa Ramadhani kutakuwa na futari/Chakula cha pamoja jioni ya siku hio ambapo viongozi na wachezaji wote wateweza kuhudhuria kwapamoja.

Den Heijer anakuwa ni kiongozi wa pili wa O.F.A kutoka Ulaya kuwasili nchini kwa malengo ya kuindeleza academy hio,mwezi uliopita kiongozi mwingine wa O.F.A Nassor ambae anaishi nchini Turkey alikuwepo nchini ambapo alikuja na jopo la waandishi wa TV ya TRT Tv International ya nchini humo ambapo waliweza kufanya video na vijana hao wa O.F.A video ambayo iko katika matayarisho ya mwisho kabla ya kurushwa hewani kwenye Tv hio inayoonekanwa kote barani ulaya pamoja sehemu nyingine nyingi duniani.

wiki ijayo kiongozi mwingine wa O.F.A kutoka mjini Belfast ambae ni Vice President Muddy atafika nchini ambapo katika mikakati ya viongozi wote ni kuipeleka academy hio ya O.F.A miezi michache ijayo nchini Nothern Ireland katika mashindano ya Milk Cup vile nchini Turkey ambapo wakiwa huko wataweza kucheza mechi kadhaa za kirafiki na timu za vijana za nchini humo.Lengo ni kuwatangaza vijana wake na kuonekanwa na timu za huko ili kuwapatia soko katika timu za nje

hivi sasa vijana wapo katika mapumziko kuupisha mwezi wa Ramadhani,ambapo wataanza tena mazoezi Rasmi mara baada ya mwezi huo kumalizika.
-------------------------------------------------------------------------------------------------