WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Sunday 23 May 2010

BAADA YA KUSUBIRI MIAKA 45 INTER YATWAA UBINGWA WA BARA LA ULAYA

.........................................................................................................................................................................

........................................................................................................................................................................
.........................................................................................................................................................................
Inter Milan jana walitwaa ubingwa wa mabingwa wa bara la ulaya baada ya kusubiri kwa zaidi ya miaka 45.

Alikuwa ni mshambuliaji hatari wa Inter kutoka Argentina Milito baada ya kupachika mabao yote mawili muhimu kwa timu yake ya Inter na kuifanya inter kuandika historia ya kuwa timu ya sita ya barani ulaya kutwaa makombe matatu kwa msimu mmoja.

inter kutokana na ushindi huo imeweza kupiga "A HAT-TRICK" msimu huu baada ya wiki iliyopita kutwaa ubingwa wa ligi ya Serie A na kombe la Taifa la nchi hio (F.A cup).

Inter sasa inajumuika na timu nyingi 5 kufanya idadi ya timu sita za bara la ulaya kutwaa makombe 3 kwa msimu mmoja ambazo ni Celtics Glasgow 1967,Ajax Amsterdam 1972,PSV Eindhoven 1988,Manchester United 1999,na F.c Barçelona msimu uliopita 2009 pamoja na Inter Milan msimu huu 2010.

Mbali na record hio ya Inter kocha wao pia Jose Morinho ameweza kupanda daraja zaidi kwa kuandika Record nyingine katika soka kwa kuwa kocha wa 3 barani ulaya kutwaa ubingwa wa Champions League mara 2 wakiwa na timu 2 tofauti.

kabla ya pambano la jana record hio ilikuwa ikishikiliwa na Ernst Happel alietwaa ubingwa huo na Timu ya Feyanoord Rotterdam ya Holland mwaka 1970 kabla kutwaa tena ubingwa huo na Hamburg S.V ya Ujerumani mwaka 1983 miaka 13 baadae.

baadae kocha maarufu Ottmar Hitzfeld alitwaa ubingwa huo na timu ya Borusia Dortmond mwaka 1997 na baadae 2001 alirejea historia hio akiwa na Bayern Munich timu zote
mbili kutoka nchini ujerumani.

Jose Morinho jana aliandika historia hio pia baada ya kukamilisha idadi ya makocha hao pale alipotwaa ubingwa huo na F.C. Porto mwaka 2004 na msimu huu 2010 Inter Milan.

Mchezaji Samuel Eto ó ameweza kujiandikia record yake baada ya kutwa ubingwa huo wa bara la ulaya mara 3 ndani ya miaka 4,

aliweza kutwaa ubingwa huo miaka 4 iliyopita mara mbili aliwa na F.c Barçelona na msimu huu 2010 akiwa na Inter Milan.
........................................................................................................................................................................