WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Monday 31 May 2010

KOCHA ABDULGHAN MSOMA AKUTANA NA CHIPUKIZI WA ORANJE FOOTBALL ACADEMY

Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ambae pia ni kocha mtaalam wa soka nchini Abdulghan Msoma wiki iliyopita alikutana na wachezaji wa Oranje Football Academy mazoezini na kuzungumzia mambo mengi ambayo chipukizi hao wanatakiwa kuyafata ili kuweza kufikia katika kiwango kinachotakiwa.

Katika aliyozungumzia ni pamoja na nafasi muhimu katika timu ambayo ndio inayofanya timu nzima kupangilia mchezo ambapo ni nafasi ya Goal Keeper, Kocha Msoma alifafanua kuwa kipa ndio mchezaji wa mwisho ambae anawaona wachezaji wa timu zote mbili zikiwa kiwanjani,
na ni mchezaji pekee anaewaona wachezaji wote jinsi walivyojipanga wakati wa kushambulia na kushambuliwa,kwa hio ni jukumu la makipa kuweza kuwa makini kuipanga timu ili kutosababisha kukatika katika safu ya ulinzi na kutoa mwanya wa kufungwa kizembe.

mbali na nafasi ya kipa kocha Msoma alizungumzia nafasi zote katika timu na umuhimu wake ,pamoja na nidhamu kuwa ni muhimu sana kwa mchezaji wa soka , katika hatua nyingine aliwapa nafasi ya Credit D kwa muono wake kwa chipukizi hao wa Oranje Football Academy.

Mwisho aliwasifia vijana hao kwa kuwa na Skills za hali ya juu na kujiamini wakati wakiwa kiwanjani na ndio inayosababisha kutulia na kutandaza soka kwa kujiamini na kupelekea kutobabaika hata pale inapotokea kuwa tumefungwa bao hio kuwafanya vijana wetu kutulia zaidi na kukomboa na pia kuibuka na ushindi. hii ni ilikuwa ni nafasi nyingine kwa vijana wa Oranje Football Academy kukutana na kocha Msoma vilevile ikiwa ni mara nyingine tena kwa chipukizi hao kupata mafunzo ya walimu wataalam wa soka.
.................................................................................................................................................................