WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Monday 31 May 2010

UONGOZI WA ORANJE FOOTBALL ACADEMY WAKUTANA NA UWAKI TAYARI KWA KUANZA KAZI KWA PAMOJA

kiongozi wa Oranje Football Academy jumamosi ya wiki iliyopita ilikutana na Uongozi mzima wa UWAKI tayari kuanza kazi kwa Organisation hio na kituo cha kukuza soka kwa vijana nchini Oranje Football Academy.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika mji wa Amsterdam nchini Holland ambacho kilifanyika katika Restaurant ya WOKKING chinese iliyopo katika mtaa wa Buikslotermeer Plein 15-17 ambapo awali viongozi hao walipata dinner iliyoandaliwa na uongozi wa Uwaki.

Kikao hicho ambacho kilianza saa 1 usiku na kumalizika saa 4:15 usiku kilizungumzia mambo mengi ya maendeleo ikiwemo mipango ya kituo cha O.F.A.

Katika yaliyozungumziwa ni mpango maalum wa kukiimarisha kituo hicho na kukifanya kiwe na nyota wengi kwaajili ya kucheza soka nje. katika mpango ambao utaanza kufatiliwa hivi karibuni ni kukisajili kituo hicho cha O.F.A na kukipatia uanachama katika chama cha soka cha KNFB (Kingdom of Netherlands Football Bond) kwa kupotia kwa Uwaki.

Hii itasaidia kwa vijana wetu hapo baadae kuwaombea misaada mingi ya kisoka kutoka katika chama hicho cha soka ikiwemo ya kuwaomba makocha na wataalam wa soka kutoka holland kuja nchini kuwapatia mafunzo mbalimbali ya kisoka, aidha kuwaalika walimu wetu kwenda kupatiwa mafunzo nchini holland pamoja na kuomba mialiko ya mara kwa mara kwa vijana wetu wa O.F.A kwenda nchini holland kushiriki mashindano mbalimbali ambayo hufanyika nchini humo kila mwaka na kuzishirikisha timu nyingi za vijana kutoka mataifa mbalimbali duniani kwa lengo la kuwatangaza na kuwapatia soka nchini humo.

Kwa upande mwingine akiongea katika kikao hicho President wa Uwaki ndugu Sunday alisema kuanzia tarehe ya kikao hicho wataanza kushirikiana na Wakala wetu wa soka anaetambuliwa na Fifa ndugu Ali Saleh ili aweze kuwa katika maagent wazuri watakaosaidia maendeleo ya soka nchini.

katika ambayo yameanza kufatiliwa kuanzia hivi sasa Agent huyo wa Fifa Ali saleh ataweza kupewa kuwasajili katika uwakala wake vijana zaidi ya 10 wenye umri kati ya miaka 10-20 ambao wanasakata soka nchini holland katika vilabu mbalimbali hivyo itamfanya agent wetu kuwa tayari na zaidi ya wachezaji 10 ulaya ambao wanacheza soka ya kufundishwa ya kitaalamu katika vilabu vyao wanavyochezea hivi sasa,

karibuni uongozi wa Uwaki/O.F.A uliopo Holland utawasiliana na Ali Saleh ili kuanza rasmi kazi ya kuwasajili wachezaji hao nyota wanaosakata soka ulaya na hio kupelekea kupanda katika safu ya juu kwa agent huyo kuwa ni mmoja kati ya agent mwenye wachezaji wengi ulaya .

Katika wachezaji hao agent huyo wa kituo hicho cha kukuza soka kwa vijana nchini ataweza kumnyakua nyota wa soka wenye umri wa miaka 14 anaechezea katika timu ya taifa ya U/14 ya Holland.

kutokana na mpango huo kiongozi huyo wa O.F.A ambae pia ni agent wa fifa na mwandishi wa habari wa sauti ya BBC Swahili ataweza kupata urahisi wa kukutana na vilabu vyote wanavyochezea wachezaji hao ambapo ataweza kujitambulisha juu ya wachezaji wake wanaochezea katika vilabu vyao vilevile ataweza kuanza urafiki mzuri na vilabu hivyo na kuanza kuwatangaza vijana wengine nchini kwaajili ya kujiunga na vilabu hivyo.

Katika hatua nyingine ambayo Uwaki itaifanikisha hivi karibuni ni kuwasajili wachezaji wote wa timu ya soka ya Uwaki iliyopo nchini Holland na kumfanya Agent wetu huyo kuvuna Timu nzima ya wachezaji vijana wenye vipaji waliopo ulaya,

zaidi ni kuanza kufatilia wachezaji wote nyota wanaozungumza lugha ya kiswahili wenye vipaji vya hali ya juu na kuweza kuiboresha na kuanza kuiandaa timu ya uwaki katika sura mpya ambapo siku za mbele kuweza kutoa nyota wengi pamoja na kuchukua nyota wengine nchini na kwenda kufanya stage na vijana hao wa Uwaki ambapo mpango utaandaliwa ili kuwaalika makocha/Scouts wa vilabu mbalimbali nchini Holland kuangalia na kujichagulia wachezaji nyota kutoka hapo ambapo mpango huo utakuwa ukiendelea mara kwa mara hadi kufikia lengo la kutoa wachezaji wengi nchini kucheza soka katika bara la ulaya.

Kwa kumalizia President sunday alisema tayari kuanzia muda huu ataanza kufatilia vifaa vya timu yetu ya vijana ya Oranje Football Academy itakayokuwa na maandishi ya Uwaki vifaa ambavyo vitakuwa na rangi za academy hio Oranje,nyeupe,blue,na nyeusi

Mwisho wataalamu weu wa soka waliopo nchini Holland watakuwa wakiwasiliana na viongozi wa O.F.A waliopo nchini ili kubadilishana utaalam na kuwaweka vijana wetu katika sura mpya soka la kisasa.

katika ambayo yatafatiliwa ni mchezaji wa U/17 atakae pata mjeruhi au kuugua mara baada ya kurejea katika hali ya kawaida atatakiwa kwanza aanze mazoezi mepesi na vijana wa U/14 ili aweze kurejea taratib katika hali yake ya kawaida kabla ya kukutana na miamba wenzake wa U/17 ambapo kumrejesha mchezaji moja kwa moja katika timu kubwa wakati akitoka katika majeruhi inaweza kmsababishia mchezaji ku risk na inaweza kumsababishia kupata majeruhi mengine kwavile mwili utakuwa haukurejea katika hali ya kawaida.

Aidha kutakuwa na mchakato mzima baada ya kimalizika ligi na kuangalia uchezaji wa kila mchezaji msimu mzima, kutakuwa na wachezaji ambao viwango vyao vimeshuka ambao wanahitajika katika academy hio hapo baadae ambapo wataweza kukodishwa kwa timu nyingine za vijana kwa lengo la kupata nafasi za kucheza mechi nyingi kabla ya kurudi katika academy yetu akiwa "fiti"

mipango pia itafanywa hapo baadae kabla ya kuanza msimu kutaandaiwa Trial kwa vijana ambao watakuwa viongozi wetu wana scout katika mchi zote za ligi ya vijana,
lengo ni kuchukua vijana wataopata nafasi ya kucha katika academy na sio kuwaweka bila ya kupata nafasi ya kucheza na kupelekea kuwapotezea viwango vyao ambapo wachezaji vijana wanatakiwa kupata mechi kila wiki ili kuweza kuongeza skills yake.

hayo machache ni katika ambayo wataalam wetu wa soka waliopo holland wataweza kuwasiliana na viongozi na jopo la makocha wa O.F.A siku zijazo kuhakikisha tunatoa wachezaji wenye uwezo mkubwa kisoka hapo baadae
....................................................................................................................................................................