WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Wednesday, 2 June 2010

NYOTA WA ORANJE FOOTBALL ACADEMY SEIF ABDALLA"KARIHE" KUZAWADIWA TUNZO YA UCHEZAJI BORA


nyota wa Oranje Football Academy seif Abdalla"karihe" (pichani katikati) amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa kituo hicho na kufanikiwa kutwaa tunzo maalum.
..........................................................................................................................................................
.....................................................................................................................................................................
Uongozi wa Uwaki/OFA uliopo Holland umemchagua mshambuliaji nyota wa Oranje Football Academy Seif Abdalla"Karihe" kuwa mchezaji bora wa kituo hicho cha kukuza soka kwa vijana nchini.

Nyota huyo ambae aliitwa katika timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania ya U/17 pamoja na kutokuwemo katika listi ya mwisho ya wachezaji wa vijana wa Taifa iliyokwenda nchini South Africa wiki hii hio haifanyi nyota huyo kukosa tunzo hio.

Nyota huyo anaevaa jezi number 7 ya Oranje Football Academy emekuwa ni mchezaji wa kwanza wa kituo hicho cha Oranje Football Academy kuchaguliwa kujiunga na timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania kwa mara ya pili mfulululizo, mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka jana ambapo alishiriki katika mashindano ya kombe la challenge ya vijana U/17 yaliyofanyika nchini Sudan.

Tunzo hio ya aina yake itamfanya nyota huyo kuwa nyota wa kwanza katika historia ya kituo hicho cha kukuza soka kwa vijana kuteuliwa kutoka kwa viongozi wa Uwaki/O.F.A tokea kuanza kazi kwa pamoja mapema wiki hii.

Utaratibu huu utakuwa ukifanywa kila mara baada ya kumalizika msimu ya ligi na tunzo mbalimbali zitatolewa kwa wachezaji bora/nidhamu/wafungaji na makipa bora kwa pande zote mbili U/14 na U/17 ambapo Uwaki/O.F.A waliopo barani ulaya watashirikiana na viongozi wenzao waliopo nchini ili kuweza kuwapata wachezaji ambao wataweza kuwa na sifa za kupata tunzo hizo.

Tunzo hii ambayo itakuwa ni kama linavyooenekana kombe la Dunia imetolewa maalum kwa mshambuliaji Seif Abdalla ili kuwa kumbukumbu kwake ya kupokea tunzo hio katika safari yake yote akiwa mwana soka,

Kutokana na kuwa hivi sasa Africa inaiwakilisha dunia nzima katika mashindano ya kombe la Dunia yatakaoanza wiki ijayo nchini South Africa viongozi wetu wa Uwaki/O.F.A wameona kumbukumbu ya mwaka huu ya kombe la dunia itakuwa ndani ya historia za watu wengi hio imeweza kumuandalia nyota wake kumbukumbu hii nzuri ya aina yake ambayo itamfanya kutosahau fainali za kombe la dunia za mwanzo kufanyika nchini Africa kutokana na tunzo hio.

Tunzo hio inatarajiwa kutumwa hivi karibuni kwa viongozi wa O.F.A waliopo nchini ili kuweza kumpatia nyota huyo mwenye uwezo wa hali ya juu kisoka ambae ni tegemeo la taifa hapo baadae.
KWA NIABA YA UWAKI/O.F.A INATOA PONGEZI KWA MSHAMBULIAJI SEIF ABDALLA KWA KUNYAKUA TUNZO HIO NZURI NA PIA KUWATAKIA NYOTA WENGINE KUZIDISHA BIDII ILI KUWEZA KUFANIKIWA KUTWAA TUNZO ZIJAZO.
....................................................................................................................................................................