WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Sunday, 4 July 2010

SPAIN YAIFUATA GERMANY KATIKA NUSU FAINALI

Iker Casillas-Sara Carbonero TV5 spain
.............................................................................................................................................
.........................................................................................................................................
............................................................................................................................................

Mrembo na mwandishi wa habari maarufu wa SPAIN SPORTS TELECINCO ya mjini Madrid-Spain Sara Carbonero akimuhoji Casillas mara baada ya pambano la jana mjini Johannesburg ambapo Spain ilishinda bao 1-0 dhidi ya Paraguay na kuingia nusu fainali. Sara Carbonero ni mpenzi mkubwa wa F.c Barçelona huku akiwa ni mchumba wa Casillas ambae ni kipa wa Real Madrid.

kumekuwa na kugongana maneno mara nyingi katika nyumba yao iliyopo katika jiji la madrid kutokana na Sara mara nyingi akitoa maelezo ya kuipendelea F.c Barçelona katika TV5 na kuisifia ni timu bora nchini spain na duniani kwa ujumla maelezo ambayo mara nyingi hua yanapingwa na mchumba wake, Casillas ambapo mara baada ya Carbonero kurejea nyumbani kunakuwa na mgongano wa maneno kati yao kwani Casillas anaona timu bora duniani ni Real Madrid ambapo maelezo hayo yanakataliwa na Carbonero.mara nyingi inakuwa zaidi pale ambapo Real Madrid na f.c Barçelona zinapocheza pamoja huku mwandishi huyo akitoa maelezo kwa jiansi pambano lilivyokuwa na alivyoliona yeye,suala ambalo kama ikitokea Real Madrid kupoteza pambano hilo Casillas hurejea nyumbani bila ya furaha na kukumbana na mpenzi wake akiwa na furaha tele kutokana na ushindi wa f.c Berçelana suala ambalo linaonekana kutopata ufumbuzi wowote katika nyumba hiyo.
Zaidi ni kuwa wana enjoy maisha pamoja ukiondoa mgongano huo wa maneno katika safu ya soka
..............................................................................................................................................
..............................................................................................................................................
...........................................................................................................................................
............................................................................................................................................
............................................................................................................................................
..........................................................................................................................................
Spain imefanikiwa kutinga nusu fainali ya soka ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza tokea mwaka 1974 ambapo ilicheza kwa mara ya mwisho dhidi ya holland na kufungwa mabao 4-0,
mara hii Spain itapambana na Germany katika nusu fainali itakayofanyiaka jumatano katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg baada ya jana kuifunga paraguay bao 1-0,bao la spain
lilipachikwa kimiani na David Villa katika dakika ya 83.
katika pambano hilo Paraguay ilipoteza penalti katika dakika ya 59 wakati Cardoso alipiga penalti hio iliyoishia mikononi mwa Casillas.Spain ilipata penalti pia katika dakika ya 59 penalti iliyopigwa na Xavi Alonso aliifungia spain dakika ya 61 lakini penalti hio ilikataliwa na mwamuzi kutokana na wachezaji wa Spain kuvamia eneo boksi wakati penalti hio ikiwa inapigwa hivyo kuwa usumbufu kwa kipa.mwamuzi aliamua penalti hio ipigwe tena ambapo Alosi aliepiga mara hii upande wa kushoto wa kipa Villar na kufanya kipa huyo kuipangua penalti hio.

kwa matokeo hayo timu nne bora za mashindano hayo ni kama hivi.

Holland v/s Uruguay.

Germany V/s Spain.
..................................................................................................................