Katika Mazoezi hayo ambayo Nyota hao wa Zamani kutoka barani Ulaya walivutiwa sana na Vijana Chipukizi wa Oranje Football Academy na kuandika ukurasa mpya wa kirafiki kati yao.
Mara baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo ambayo itawasaidia sana nyota wa O.F.A katika kukuza vipaji vyao vya soka kutokana na kusoma mengi kutoka kwa nyota hao wa zamani pande zote mbili zilikabidhiana zawadi rasmi kwaajili ya Urafiki na kumbukumbu kati yao.
O.F.A iliwakabidhi zawadi maalum kama ambavyo zinaonekana "pichani" wakati Bern Selection waliwakabidhi O.F.A seti moja ya jezi pamoja na mipira kumi vifaa ambavyo vitawasaidia sana O.F.A katika kuendeleza kasi yao ya maendeleo ya soka kwa vijana nchini.