Poulsen pia alitangaza kikosi cha wachezaji 16 cha timu maalumu ya chini ya miaka 17 ya Copa Cocacola kwa ajili ya ziara ya mechi kadhaa zitakazofanyika Afrika Kusini kati ya Oktoba 27 mpaka Novemba 2 mwaka huu.
Aliwatangaza wachezaji hao kuwa ni Hamadi Juma, Peter Manyika, Mgaya Abdul, Ismail Gambo, Miraji Selemani, Basil Seif, Mohamedi Hussein, Hussein Ibrahimu, Selemani Bofu, Mudathiri Abbas, Mohamedi Haroub, Farid Shaha, Mbwana Hassani, Joseph Lubisha, Paschal Matagi na Salvatory Nkulu.
ORANJE FOOTBALL ACADEMY INAMTAKIA KILA LA KHERI NYOTA WAKE KATIKA SAFARI HIO.