WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday 28 January 2012

MORROCO,NIGER ZATUPWA NJE

Waandaaji washirika wa Africa Nations Cup 2012 Gabon wakicheza kwa ari kubwa huku walishangiliwa kwa nguvu zote kutoka kwa mashabiki wa nchi hio wameitupa nje ya michuano hio Morocco katika sekunde ya mwisho ya pambano hilo.
Ilionekana kama Morocco kupata nafuu ya sare baada ya nahodha wa nchi hio Kharja kusawazisha bao la pili kwa njea ya Penalti katika dakika ya 90 lakini vijana wa Gabon walipigana hadi sekunde ya mwisho na kuitupa morocco nje ya michuano hio kwa jumla ya mabao 3-2.
morocco ilikuwa ya kwanza kuandika bao katika dakika ya 24 bao lililofungwa na nahodha wao Kharja ambae pia alifunga bao la pili kwa njia ya penalti dakika ya 90 ya pambano hilo,na yale
mabao ya Gabon yalitundikwa na Aubameyang katika dakika ya 77 wakati bao la pili lilifungwa na Cousin katika dakika ya 79 kabla ya Mbananguayu kupiga freekick iliyokwenda pembeni kona ya kushoto ya goli la Morocco katika sekunde ya mwisho ya dakika 5 za nyongeza za pambano hilo hivyo kuihakikishia nchi hio kusonga mbele hatua ya Robo fainali.
Freekick kama ile muhimu ilipigwa na David Backham kati ya England dhidi ya Greece miaka kadhaa iliyopita na kuipatia ticket England ya kwenda katika kombe la dunia yaliyofanyika nchini Japan na South Korea ambapo Greece ilihitajia sare hadi dakika ya mwisho ilipotupwa nje.

Katika pambano jingine lililofanyika mapema kati ya Niger na Tunisia lilimalizika kwa Niger 1-2 Tunisia, mabao ya Tunisia yalifungwa na Msakni dakika ya 4 na Jemaa katika dakika ya 90 ya pambano hilo wakati bao la pekee la Niger lilifungwa kwa kichwa na Ngounou katika dakika ya 9.
Tunisia na Gabon zinasonga mbele zote zikiwa na point 6 baada ya kushinda mechi zao mbili huku morocco na Niger wakisubiri kukamilisha ratiba kwa mechi yao ya mwisho na kurejea njumbani.