WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Thursday 26 January 2012

NI WACHEZAJI 2 TU WAZALIWA KIKOSI CHA EQUETORIA GUINEA

Hakuna hata mmoja wa wachezaji wa Equetorial Guinea ambao walicheza jana dhidi ya Senegal ambae alizaliwa katika nchi hio,mbali na kuwa ni timu ya chini zaidi kuingia katika mashindano hayo ya Nations Cup kuwahi kutokea katika ranki ya Fifa Equetorial Guinea wapo katika nafasi ya 151 hata hivyo kutokana na ushirikiano wa mkubwa wa nchi hio ya Equatorial Guinea imekuwa ni ya kwanza kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Mfungaji wa bao la ushindi dakika za majeruhi dhidi ya Senegal 2-1 jana Kily ambae anachezea daraja la nne nchini Spain aliweza kuitumbukiza nchi hio iliyopata uhuru wake kutoka kwa Spain kucheza katika hatu ya nane za mwisho.
Kabla ya hapo Guinea Equetorial ilishinda 1-0 dhidi Libya na kuleta mafanikio makubwa kwa nchi hio yenye idadi ya watu chini ya 700 000.
Kipa kuoka Brasil,mlinzi kutoka Liberia,kiungo mkali kutoka Ivory Coast na mshambuliaji kutoka Cameroon na wachezaji wengine kutoka Spain ambapo hakuna hata mmoja kati ya wachezaji 13 waliocheza jana ambae alizaliwa nchini Equetorial Guinea ambapo katika kikosi cha wachezaji 23 ni kipa namba 3 pamoja na Felipe Evono na beki wa hakiba tu Jose Bekung peke yao ndio waliozaliwa katika nchi hio ambayo inafundishwa na kocha kutoka nchini Brasil.
Katika sera ya kocha Antonio Dumas kutoka Brasil aliwataka viongozi na maofisa na wanasiasa kuimarisha kikosi cha nchi hio kwa kuwatumia wachezaji wanaochezea nje ya nchi ili kuweza kuleta mafanikio katika nchi hio ambapo pia aliwapa mfano kwa baadhi ya yalifanywa na nchi ya Togo wakati alipokuwa kocha wa nchi hio.
Baada kukubaliana na mawazo yake Dumas wakubwa wa nchi aliwaalika baadhi ya wachezaji kadhaa kutoka nchini Brasil kuchukua uraia wa nchi ili kuweza kuchezea na kukiimarisha kikosi cha nchi hio na baadaye kuipanua sera hio kuita kuchukua wachezaji pia pamoja na mataifa mengine.
Katika hatua nyingine Nchi hio ambao ni koloni la zamani la Hispania, waliona kuwa ilikuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa kulikuwa na wachezaji wenye asili ya Equatorial Guinea ambao wamezaliwa na kucheza katika nchi ya Hispania hivyo kuwaita wachezaji kadhaa waliozaliwa na kucheza soka nchini hispania kama watoto wa asili yao ya Equetorial Guinea,lakini kama hilo pia halitoshi kuimarisha kikosi chao walimualika mchezaji yeyote ambaye alikuwa tayari kupata uraia wa nchi hio.
Mlinzi mkali na kikosi hicho ambae jana alipewa kadi nyekundu Lawrence Doe ambae awali alikuwa na matumaini ya kuwa na uwezo wa kucheza soka ya kimataifa kwa ajili ya Liberia nchi yake ya asili ,lakini alijikuta ndoto zake hizo kwamba zilishindikana na hivyo kuamua badala yake kuichezea Equetorial Guinea badala ya Liberia.
Katika mahojiano Beki huyo alisema "Mimi ni M'Guinea, wao wananitunza,na serikali hapa mimi inanitunza vizuri," aliwaambia waandishi wa habari. "Najisikia furaha sana na kiburi sana kwa sababu hata kama mimi nimezaliwa Liberia lakini sasa mimi niko Guinea,Equetorial Guinea ni nyumbani kwangu., Nina mke wangu na mtoto wangu hapa sasa."