WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Wednesday, 25 January 2012

ORANJE FOOTBALL ACADEMY YAITAHADHARISHA MAFUNZO

Oranje Football Academy inawatahadharisha mabingwa wa Zanzibar Mafunzo f.c kujitayarisha vikali kutokana na kukabiliwa na timu ngumu katika pambano lake la awali la michuano ya Caf Champions League pambano ambalo Mafunzo wataanza nyumbani tarehe kati ya tarehe 17-18-19 mwezi 02-2012 dhidi ya Liga Muçulmana ya Maputo kutoka Msumbiji.
Kutokana na jina geni na mara ya kwanza kushiriki michuano hio mikubwa kwa vilabu barani Africa timu hio kutoka katika jiji la Maputo ambayo imeanzishwa miaka ya karibuni tu imeweza kuleta mafanikio makubwa katika soka nchini Msumbiji,kutokana na utajiri wa timu hio, mipango mizuri ,heshima kwa wachezaji na viongozi wote imeifanya timu hio kuwa kubwa kisoka kuliko timu zote za nchi hio kwa sasa.
Mbali na kuwa na agent wake wa fifa katika club hio ambae ni Agent wa mlinzi mkali Simao Mathe wa Panathinaikos ya nchini Greece agent ambae pia anawachezaji kadhaa wanaosakata soka sehemu mbalimbali duniani pia mmiliki wa timu club hio ni kaka wa agent huyo anaetambuliwa na fifa.
Club hio ambao inamiliki uwanja wake wa kuchezea mechi wenye nyasi bandia za kiwango cha fifa pia kuwa na sports complex yake katika mji wa Matola nje kidogo ya mji wa Maputo.

Kutokana na uwezo wao wa kifedha na mipango bora club hio inayojulikana kama "PALMARÉS" wanaovalia jezi nyeupe na kijani imeweza kuwazoa nyota wengi vijana kutoka katika vilabu vyote vikubwa vya nchi hio pamoja na nchi nzima kwa ujumla huku wakiwa pia ina kiungo mshambuliji kutoka nchini Brasil na nyota wengine wengi kutoka sehemu nyingine Africa.
Mbali na soka ambapo wana timu ndogo zaidi ya 4 wa umri mbalimbali ambao ni nyota wanaotarajiwa kukiongozea makali kikosi hicho cha Liga Muçulmana ambao kabla ya soka ilikuwa ni timu ya FUTSAL kabla ya kuigeuza kuwa timu ya soka miaka michache iliyopita pia inaendelea na kuwa na timu kali ya FUTSAL ambapo wana Complex katika barabara ya Eduardo Mundlhane katika ya jiji la maputo karibu na barabara muhimu ya jiji hilo ya Julius Nyerere ambapo pia wana complex nyingine ya Futsal katika mji wa Chimoio uliopo mpakani na Zimbabwe.
Pamoja na michezo hio klabu hio inayoongozwa kwa utalamu wa kisasa katika kila idara pia ina michezo na timu kali za Cricket,Hockey,Basketball na Handball.

kutokana na timu hio kuwa katika uendeshaji wa hali ya juu kwa nchini Tanzania hivi sasa Azam fc wakizidi kujitahidi wataweza kufikia uwezo wa kuiendesha timu yao kama hawa Liga Muçulmana miaka michache ijayo.
Kutokana na uzito katika timu yao ya Soka O.F.A inawatahadharisha mabingwa wa Zanzibar Mafunzo wajitayarishe vikali kwani itakupambana na moja ya timu kali kwa sasa katika michuano hio ya Mabingwa wa Africa.

ratiba ya timu ya timu ya Mafunzo ni kama hivi:
17,18,19/02/2012
Mafunzo FC vs Muçulmano de Maputo

02,03,04/03/2012
Muçulmano de Maputo vs Mafunzo FC