WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Thursday, 9 February 2012

FINAL CHIPOLOPOLO VS ELEPHANTS

Kipa wa Zambia Mweene akipangua penalti ya Gyan katika dakika ya 9.
......................................................................................................................................

Zambia Chipolopolo(kwa lugha ya Bemba ni Bullet kwa mujibu wa nahodha wa Zambia Katongo)imetinga Fainali kwa kuichapa Ghana bao 1-0 na kuiwacha Ghana ikishangaa kutoamini kutupwa nje ya fainali hizo za Orange Africa Cup of Nations 2012.

Wakijiamini zaidi kucheza fainali Ghana itabidi ijilaumu kufungwa mechi hio na Zambia ambao wametinga fainali hizo kwa mara ya kwanza tokea mwaka 1994 na kupoteza fainali hio dhidi ya Nigeria.

Ghana ilipoteza Penalti katika dakika ya 8 ambapo penalti hio ilipanguliwa na mmoja wa makipa bora bara Africa Mweene.Bao pekee la Zambia lililoipeleka fainali lilifungwa na Mayuka katika dakika ya 78.

Kutokana na Ushindi wa Chipolopolo sasa itakumbana na Ivory Coast siku ya jumapili baada ya "Elephants" kuifunga mali pia kwa bao 1-0 bao lililowekwa wavuni na Gervinho baada ya kukokota mpira nyuma ya mstari wa kati kushoto na kuingia nao hadi ndani ya sanduku la hatari la Mali na kuandika bao katika dakika 44 bao ambalo lililotosha kwa Ivory Coast kutinga fainali dhidi ya Zambia.

Mali na Ghana zitachuana siku ya jumamosi kutafuta mshindi wa tatu wa mashindano hayo ya Can 2012.