WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Thursday 9 February 2012

VILABU NCHINI MFATILIENI HUYU KINDA WA ZAMBIA EVANS KANGWA

Katika kikosi cha Zambia kinachoshiriki Fainali za Africa Cup nchini Gabon na Equetorial Guinea kuna kinda wa miaka 17 Evans Kangwa anaechezea soka nchini Zambia katika klabu ya (Nkana FC),ambapo vilabu vingi vikubwa nchini South Africa vikiwa katika radi kubwa za kumtwaa kinda huyo ambae wataamau wengi wa soka barani ulaya tayari wamemwagia sifa sana kwa uwezo wake.Kinda huyo ambae vilabu vya Orlando Pirates na Bucs za mji wa Soweto nchini South Africa.

Nyota huyo alingára sana katika michuano ya Cosafa Youth Championship U20 iliyofanyika mwezi dec 2011 nchini Botswana amevivutia vilabu vingi kutokana na uchezaji wake pamoja na upachikaji mabao.

Hivi sasa kinda huyo ameonyesha uwezo mkubwa na hadi sasa tayari amepachika mabao 17 katika ligi ya Zambia hivyo kumfanya kuwa ni mmoja wa washambuliaji wanaotisha nchini Zambia kwasasa huku kinda huyo akiwa bado na umri mdogo zaidi.

Kwa Vilabu vya nchini huyo Kinda ndie wa kumfuatilia kwa sasa kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kufanya hivyo ambapo ataweza kuwasaidia sana katika klabu hio na tayari kinda huyo bado ana muda mrefu wa kucheza soka na vilevile kila atakapozidi kungára katika klabu yoyote nchini soko la kinda huyo litazidi kupanda hivyo kuifanya klabu itakayomtwaa kujitengenezea kipato kizuri na huku nyota huyo akiwasaidia katika michuano mbalimbali atakayoshiriki na klabu hio nchini. Nadhani hivi sasa ni wakati mzuri vilabu nchini kuangalia kutwaa vijana wengi ndani na nje ya nchi ili kuweza kujijengea mafanikio ya muda mrefu kama vilabu vya Tp Mazembe ambao wana wachezaji 4katika kikosi cha Zambia kilichoingia fainali za Africa Cup of Nations kuna wachezaji Walinzi: Stopilla Sunzu, Hichani Himonde, Francis Kasonde (TP Mazembe Englebert, DR Congo),na kiungo:Rainford Kalaba (TP Mazembe Englebert, DR Congo),


Nyota hao wamezidi kuwiva na wataweza kutoa mchango mkubwa zaidi wataporejea katika klabu yao kutokana na uzoefu wa kukumbana na wachezaji wakubwa mbalimbali wenye majina mazito hivyo wataweza kujijengea uwezo mzuri wa kujiamini wakiwa kiwanjani ambapo hio ndio silaha kuu ya ushindi katika masuala yote duniani sio kisoka tu pia nyota hao kutokana na kuwa na umri mdogo ni hazina ya muda mrefu kwa Tp Mazembe pia mipango ambayo hufanywa na vilabu vingi vya North Africa pamoja na Ulaya na South America kwa ujumla.

Chanzo chetu cha O.F.A kupitia EuroSports Tv na kabla Sports1 Tv kimeweza kupata habari hizi za nyota Evans Kwanga kutoka kwa wataalamu mbalimbali ambao wamefananisha na Jackob Mulenga mfungaji bora wa timu ya Taifa ya Zambia anaecheza soka ya kulipwa nchini Holland katika klabu ya F.C Utrecht ambapo hivi sasa anamajaraha ya muda wa miezi kadhaa hivyo kutomruhusu kushiriki katika fainali hizo za Can 2012.

O.F.A inatoa ushauri kwa vilabu nchini kuwa Evans Kwanga ni mchezaji wa kumuangalia kwa sasa na kumtwaa ambapo klabu itakayoweza kumchukua itakuwa imejiwekea hazina kubwa ya kuongeza kipato chake kutokana na kuwa kinda huyo yuko njiani kuelekea safari ya kuwa nyota mkubwa hivi karibuni.