WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Wednesday 1 February 2012

GABON YAITUNGUA TUNISIA 1-0

Bao lilifungwa na Aubameyang katika dakika ya 62 lilitosha kuipeperusha bendera ya Gabon kushika nafasi ya kwanza baada ya kuichapa Tunisia bao 1-0 pambano lililofanyika katika uwanja wa Stade de Franceville.
Nyota huyo anayechezea soka ya kulipwa nchini ufaransa katika klabu ya Auxere ambae baba yake alikuwa ni kocha wa timu ya taifa wa nchi hio iliyoshiriki kwa mara ya kwanza fainali hizo za kombe la mataifa ya africa za mwaka 1994 na kaka zake wawili wanaosakata pia soka ya kulipwa Lili na Katalina wakiwa hawakuitwa katika kikosi hicho cha Gabon aliweza kutundika bao hilo muhimu huku wakicheza kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Franceville ambapo pambano hilo lilihudhuriwa pia na Rais wa nchi hio Omar Bongo na mke wake raia wa Ufaransa Sylvia kushuhuhudia vijana wao wakimaliza kwa ushindi hivyo kuendeleza furaha ya nchi hio ndogo yenye idadi ya watu milioni moja na nusu na kujijengea ari zaidi kwa hatua ya Robo Fainali.

Katika pambano jingine la kukamilisha ratiba Morocco imeifunga Niger bao 1-0 kwa bao lililofungwa na Belhanda katika dakika ya 79.
Niger wanarejea nyumbani na mikono mitupu baada ya kupoteza mechi zote 3 za mashindano hayo.Wakati huohuo Serikali ya Niger imewapongeza raia wake kwa kujitokeza kwa wingi kutuma sms maalum zilizobuniwa na kuuzwa kwa beo ya $ 0.50ct kwaajili ya kuwaongezea kipato zaidi wachezaji wa nchi hio ambao walikuwa wakishiriki mashindano hayo ambapo waliweza kuvuna fedha nyingi sasa na hivyo zimesaidia sana kuwalipa mishahara wachezaji wa nchi hio na kupunguza mzigo mkubwa wa kuwabana serikali peke yake ya kulipa mishahara ya nyota wa nchi hio.