WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Wednesday 22 February 2012

HAKUNA MECHI ZA NYUMBANI KWA SIMBA NA YANGA

Katika mahojiano na baadhi ya wadau wa soka wanaoishi nje ya nchi kupitia katika blog hii inayomilikiwa na kituo cha kukuza soka kwa vijana nchini Oranje Football Academy wadau wengi wamedai kutokuwepo kwa mechi za nyumbani kati ya timu za Yanga na Simba kutokana na uhasama wa mashabiki wa timu hizo ambao wana haki za kufanya hivyo kutokana na upinzani wa timu zao.
"chukulia Liverpool au Manchester United moja wapo inabidi ichezee mechi yake ya kimataifa katika uwanja wa mwenzake na mashabiki wa uwanjani pale karibu asili mia kubwa ya mashabiki ni ya wale wapenzi wenye uwanja ambao timu yao haichezi,unadhani watawashangilia maadui zao?"aliongea mmoja wa mdau kutoa mfano kutokuwa na kila timu na uwanja wake kati ya Simba na Yanga hakutoleta mafanikio yoyote katika soka kwa vilabu hivyo kutoka na kuwa kila inapocheza moja ya timu hizo mpinzani wake anakuwa ni mshangilia wa nguvu wa timu za kigeni,timu zote zimekuwa na tabia hizi kwa miaka yote na hakuna hata mmoja wao wa kumlaumu kutokana na kufanya hivyo kwani kila mmoja anakuwa analipa kisasi cha mwenzake,
huwezi kumpata au kumlaumu ni nani alianza tabia hiyo kwani timu hizo kubwa ni za zamani sana na mchezo huo mchafu haukuanzia leo,na pia sio rahisi kuwabadilisha mashabiki wa timu hizo kutofanya hivyo kutokana na kuingia uwanjani hapo kwa tiketi zao na wana haki ya kuishangilia timu wanayoipenda wakiwa hapo uwanjani".alimalizia mdau huyo kwa maoni yake.

Katika kuchangia nini cha kufanya ili timu za nchini kuweza kufanya vizuri kujisikia zinacheza nyumbani na sio mechi zote mbili kuonekana kama wanachezea ugenini, mdau mwingine alisema "kutokana na kuwa timu zote zinatumia uwanja wa Taifa,kila mtu ni mwana wa taifa,na kila mtu anahaki ya kushabikia timu anayoitaka,hivyo ni vigumu kumzuwia shabiki wa timu pinzani kutoishangilia timu ya nje ambapo hio ni hasara kubwa kwa timu za nyumbani,kutokana na timu zetu kutofanya vizuri mara kwa mara ndio maana inapelekea timu zetu kuwa ni kidogo katika mashindano ya Caf tofauti na nchi nyingine ambazo wana timu 2 au 3 kutegemea mashindano gani kati champions league na confederation cup ambayo sisi tunapeleka timu moja kila mwaka hio ni hasara kwa vilabu vya nchini sio tu kupata maendeleo kama wenzao wa nchi nyingine bali hata kimaendelo ya soka kwa timu ya Taifa kutokana na kukosa timu nyingi zinazokutana na kutoa upinzani kwa timu za nchi nyingine.
aliendelea mdau huyo kwa kusema,kutokana na vilabu hivyo vya Yanga na Simba kuchezea uwanja mmoja hio sio tatizo kubwa kwani hata Ac Milan na Inter Milan wote wanachezea katika uwanja wa San Siro,
lakini kutokana na usimamizi mzuri utakuta hata yale mabango ya biashara yanayoidhamini Inter Milan hayakutani na wadhamini wa biashara wa Ac Milan hivyo kila timu kujikuta inacheza katika uwanja wa nyumbani kwa siku inapokuwa uwanjani hapo,hakuna siku ambapo timu inajikuta inachezea nje wakati inahitajika ichezee nyumbani.
Kutokana na utaratibu wa timu zote kila moja kuwa na uwanja wake wa nyumbani,inapocheza Inter Milan wanakuwa na uhakika ticket zao ni kwaajili ya wapenzi wao,na zilizobakia ni kwaajili ya wageni sawasawa na vilabu vingine wakichezea nyumbani wanavyouza ticketi zao kwa mashabiki wao na wageni kupewa nafasi kidogo na kuzifanya kelele za wageni hao kumezwa na umati wa timu ya nyumbani kwa siku ile,na mfano huohuo ni kwa AC Milan inapochezea nyumbani,na hata kama timu hizo zitakutana wenyewe kwa wenyewe katika uwanja huohuo wanaoutumia kama uwanja wa nyumbani ticketi huuzwa asilimia kubwa kwa ile timu inayokuwa imepangiwa kuwa timu ya nyumbani kwa pambano lile na ticketi kiduchu huuzwa kwa ile timu ya wageni kati ya hizo mbili kwa mechi hio,
hivyo kuzifanya timu hizo hata zikikutana kuna moja inakuwa ya nyumbani na moja inakuwa ni ya ugenini,kwavile wanajua kama ticketi zitauzwa tu kiholela kwa anaetaka katika jiji la Milani,huenda Inter Milan kama wanachezea nyumbani wakajikuta mashabiki wao hawazipati ticketi hizo na kuingilia ndani ya uwanja huo hivyo kujikuta pengine wanachezea nyumbani lakini mashabiki wa Ac Milan ndio wenye ticketi zote mikononi hivyo Inter kujikuta wakizomewa na kuonekana pengine wakichezea katika uwanja wa ugenini hali ya kuwa wapo nyumbani,
na hii ndio inayowaathiri vilabu vya nyumbani." alimalizia mdau huyo.

Mdau mwingine alitoa mchango wake kwa kusema"ili kuepukana na hizo tabia chafu za mashabiki wa soka nchini kuwashangilia wageni zaidi kuliko wenzao wa nyumbani ni lazima kuwe na utaratibu mzuri wa kuuza ticketi kwa klabu husika kuuzia tiketi mashabiki wake fungu kubwa la tiketi hizo na zitakazobakia kuuzwa kwa mashabiki waliobakia katika mechi za kimataifa",aliendelea kwa kusema"Nashangaa vilabu kama Simba na Yanga vina wapenzi na mashabiki zaidi milioni 8 nchini kila mmoja wao,lakini wanashindwa kuandaa mpango kila timu kupata mashabiki elfu 30 au 40 kuwauzia ticketi katika mechi zao za kimataifa?"
Kama wanasimamia vizuri basi wanaweza kufanya hivyo aliongeza mdau huyo na kumalizia"wanaweza kuuza ticketi zao kupitia kwa viongozi wao wa matawi yao ndani na nje ya mji na kuandaa utaratibu mzuri wa mashabiki wao walioko nje ya mji kufika kuhudhuria mapambano yao na kuzisaporti timu zao kwa nguvu zote,kama wataweza kuuza ticketi katika matawi yao kwa acounti za klabu zao na viongozi wa matawi kupeleka idadi ya mashabiki mwezi mmoja kabla ya pambano hadi wiki moja kabla ya mchezo basi wataweza kuuza ticketi hizo hata kabla ya siku ya mchezo na kujua ni idadi gani ya mashabiki wao watakaokuwepo kiwanjani na ticketi ngapi wauze kwa mashabiki waliobakia huku viongozi wa matawi wakiwa wawakilishi wa mashabiki na orodha ya idadi ya ticketi walizotaka na kwenda katika makao makuu ya klabu hizo kuchukua ticketi za mashabiki kila mmoja na idadi aliyoagizia na kulipia klabuni hapo tayari kwa ajili ya kushabikia vilabu vyao na kuwacha tabia ya kushangia wageni,kwa mfano"
alimalizia mdau huyo mpenzi wa moja ya klabu unayoipenda wewe hapo nchini.