WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Sunday 19 February 2012

YOSSO ANAETAYARISHWA KUJA KUWANYANYASA AKINA MAKUMBI JUMA.JUMA MGUNDA,NA MOGELLA WETU.

Kinda Babacar El Hadji Khouma miaka 18 akiwa na shirt ya timu yake mpya ya Real Racing Santander ya Spain.
......................................................................................................................................

Babacar El Hadji katika akijaribu kumtoka Granéro na Varan huku Marcelo akiangalia kwa makini kuhakikisha Yosso haleti madhara katika lango lao katika pambano la Ligi ya Spain lililofanyiaka jana katika uwanja wa Santiago Bernabéu na Real kushinda jumla ya mabao 4-0 hivyo kuongoza ligi hio kwa jumla ya point 13 mbele ya Barçelona ambayo ina mchezo mmoja mokononi.

............................................................................................................Babacar wa kwanza kulia jezi nyeusi,akisubiri kumsaidia mshambuliaji mwenzake wa Racing Santander Arana huku wakichungwa na mabeki wa Real Madrid Varan(19) Ramos,Pepe na Benzema katika pambano la La Liga

......................................................................................................................



Babacar Khouma akiwa na Fiorentina
...........................................................................................

El Hadji Babacar alipokuwa na timu yake ya Fiorentina ya Italia
.....................................................................

Babacar El Hadji akiwa na jezi ya Real Racing Santander ya Spain
......................................................................

Wakati kikosi cha Senegal kikiwa kimesheni nyota wanaosakata soka ya kulipwa nje wenye vipaji vya hali ya juu,pamoja na kikosi hicho kutofanya vizuri katika mashindano yaliyopita ya CAN 2012 yaliyomalizika hivi karibuni,ukweli ni kuwa kikosi chao kikosi kikubwa sana na kitaendelea kutisha katika soka la Africa kwani hata nchi kama Egypt,Nigeria,Cameroon,Algeria ambazo hazikuingia kabisa katika fainali za michuano hio bado nchi hizo zinaendelea kuwa na nyota wakali ukilinganisha na nchi zetu.

Huku mipango mibaya na matayarisho mabovu katika maendeleo ya soka kwa vilabu vya vijana pamoja na timu za Taifa za vijana nchini wenzetu wanaziti kupaa kutengeneza majeshi vijana katika nchi zao ambao ndio watakaokuja kupambana na wachezaji tunaowaita "nyota wa Taifa".

Kama kawaida ya Taifa letu kuendelea kuwa na nyota hao wa Taifa akina Makumbi Juma,Juma Mgunda,Zamoyoni Mogella wenzetu wa Africa wameanza kuwapika akika "new Demba Bá, Demba Ciccey,Mussa Sow" ili kuja kuwachapa wazee wetu "nyota wa Taifa Letu".

Pengine kutokana na jina la kuitwa "Nyota wa Taifa" wazee wetu wa timu ya Taifa Stars wamekuwa wakiborongo na kuporomoka kiwango kila juwa linapochomoza.

Katika pambano la jana tarehe 19-02-2012 Yosso Babacar El Hadji Khouma mwenye umri wa miaka 18 aliendelea kuonyesha uwezo wake katika safu ya ufungaji wa timu ya Real Racing Santander ya nchini Spain anakocheza soka ya kulipwa kwa mkopo kutoka wa klabu ya Fiorentina ya Italia ambapo amesajiliwa hivi karibuni na kucheza mechi kadhaa za ligi hio ya Spain.

Kutokana na uwezo wake mkubwa Kinda huyu pamoja na Yosso wa nchi hio wanaosakata soka nje ndio watakaokiwakisha kikochi cha nchi hio katika miaka ya hivi karibuni hivyo kuendelea kuifanya nchi kama wanavyofanya vizuri nchi nyingi za Africa kutisha katika soka sio kwa Africa tu bali kuzinyanyasa na kuzipa wakati mgumu timu za mataifa mengine makubwa duniani.