

Kipa wa Tunisia Mathlouthi aliwazawadia Ghana bao la ushindi baada ya kuutema mpira wa krosi uliomkuta Andre Ayew katika dakika ya 101 aliepachika bao hilo kirahisi na kutosha kuipeleka nchi katika hatua ya nusu fainali ambapo sasa itakubwana na Zambia na Ivory Coast itacheza na Mali ambayo mapema iliwatoa wenyeji wa mashindano hayo Gabon kwa njia ya penalti baada ya kutoka sare 1-1 katika dakika 120 za pambano hilo.
Penelti za Gabon zilifungwa na Poko,Mbanangoye,Mouloungui,Aubameyang alipoteza penalti baada ya kipa wa Mali Diakite kuokoa penalti hio na Manga aliifunga penalti ya mwisho.
Mali walipachika wavuni penalti zote 5 kwa mikwaju iliyopigwa na Diabate,Yatabare,Kante,Traore na Keita kumalizia penalti ya mwisho hivyo Mali sasa itakunana na Ivory Coast katika nusu fainali ya pili.