WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday, 10 March 2012

GOR MAHIA YAAGA MASHINDANO YA CAF CONFEDERATIONS CUP

Gor Mahia ya Kenya imeyaaga mashindano ya  mwaka huu ya CAF Confederations Cup baada ya kufungwa bao moja  0-1 na Ferroviario ya Msumbiji katika pambano lililofanyika katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.
Kwa matokeo ya pambano hilo Gor Mahia inayofundishwa na kocha wa muda Bobby Ogolla wametolewa kwa jumla ya mabao 4-0 baada kunyanyaswa jumla ya mabao 3-0 katika pambano la awali lililofanyika mjini Maputo msumbiji.

Kwamujibu wa mtandao CAF ONLINE ni kuwa Ferroviario ya Msumbiji sasa itacheza dhidi ya Simba ya Tanzania katika raundi ufuatayo.
Awali mtandao huo ulikuwa ukionyesha kuwa Simba itakutana na Setif ya Algeria wakati leo wamepachika kuwa Simba watakutana na Ferroviario ya Msumbiji.
.........................................
Katika pambano jingine la michuano hio timu ya Liga Muçulmano ya Msumbiji imeifunga na kuitoa nje ya michuano hio Mafunzo ya Zanzibar kwa kuifunga kumla ya mabao 3-0 katika pambano lililofanyika katika uwanja wao wa Liga Muçulmano uliopo Matola nje ya jiji la Maputo.
kutokana na ushindi huo Liga Muçulamno imesonga mbele kwa jumla ya mabao 5-0 kufuatia ushindi wa mabao 2-0 ilioupata hapo kabla.
bao la kwanza katika pambano la jana yalipachikwa na Telinho katika dakika ya 1,na  37 ya mchezo,kabla ya Reginaldo kupachika bao jingine  katika dakika ya 62.Timu hio inayoongozwa kwa utaalamu wa hali ya juu pia jana wanawake wa Basketball ya Primier ligi ya nchi hii walitwaa  ubingwa hivyo wataiwakilisha timu hio katika Champions league ya Basketball ya wanawake Afrika ambapo pia wanaume ni Mabingwa wa nchi hio wa mchezo huo.

Liga Muçulmana ilitawala mchezo tokea mwanzo hadi mwisho na kuifanya Mafunzo kuwa na wakati mgumu wa kumfikia kipa wa timu hio Caio ambae amesajiliwa kutoka nchini Brasil akiwa ni mchezaji mwingine wa timu hio kutoka Brasil baada ya Msrquem Nuguen Gonçalves Ferreira ambae hivi sasa anachezea soka nchini Asia.