WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday 3 March 2012

KINDA SIFAEL KWENDA ASPIRE FOOTBALL DREAMS NCHINI SENEGAL

Kinda la Tanzania laula Senegal

MCHEZAJI Sifael Orgenes Mollel (14) amechaguliwa katika mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream ambao uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwenda kituo cha vipaji kilichoko Dakar, Senegal.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema jana kuwa Mollel kutoka kituo cha Karume alichaguliwa katika mchakato wa mwaka jana uliofanywa na mng’amua vipaji vya soka kutoka Hispania kwa niaba ya Aspire Football Dreams yenye makao makuu yake Doha, Qatar.

“Mpango huo wa Aspire Football Dreams kwa Tanzania una vituo 14 na mchakato wa kusaka mchezaji mmoja kila mwaka kuhusisha vituo vyote hivyo ambapo kila kimoja kinatakiwa kuwa na watoto wasiopungua 176.

“Mbali ya Karume, vituo vingine ni Kigamboni, Kawe, Tandika, Makongo, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni, Morogoro, Bagamoyo mkoani Pwani na Tabata.

“Mollel atakuwa kwenye kituo hicho cha Dakar kwa muda usiopungua miaka mitatu na anatarajiwa kuondoka nchini Machi 6 mwaka huu. Kwa mwaka wa kwanza wazazi wake watalipwa dola za Marekani 2,500, wa pili dola 2,750 na wa tatu dola 3,000.

“Mpango wa Aspire Football Dreams ambao unafadhiliwa na mtoto wa Mfalme wa Qatar una vituo viwili vya kuendeleza watoto wenye vipaji ambayo viko Doha na Dakar,” alisema Wambura.

Alisema mpango huo unaendeshwa katika nchi 16 tofauti, ambazo ni Cameroon, Costa Rica, Gambia, Ghana, Guatemala, Ivory Coast, Kenya, Mali, Nigeria, Paraguay, Rwanda, Senegal, Tanzania, Thailand, Uganda na Vietnam.

Habarii imetoka katika gazeti la Habari leo,Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 2nd March 2012:

KWA NIABA YA KITUO CHA ORANJE FOOTBALL ACADEMY KINAMTAKIA KINDA SIFAEL KILA LA KHERI NA MAFANIKIO MAZURI,PIA KUWATAKA YOSSO WENGINE KUIGA MFANO WA KINDA HUYO ILI TANZANIA IWEZE KUTOA IDADI KUBWA ZAIDI KUPELEKA WANANDINGA WAO WADOGO AMBAO HUO NDIO MWANZO WA MSINGI MZURI WA SOKA NCHINI.
.......................................................................................................................................