WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday, 31 March 2012

RUDISHENI HADHI YA SOKA ZANZIBAR

Kituo cha kukuza soka kwa vijana nchini ORANJE FOOTBALL ACADEMY kinatoa pongezi zake za dhati kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutokana na uamuzi wake ilikusudia kwa makusudi kabisa kufufua soka Zanzibar na kuirejeshea hadhi yake kama zamani.

Kutokana na kikao kilichofanyika hivi karibuni soma zaidi katika webblog hio hapo chini ya inayo nukuu
http://othmanmapara.blogspot.com/2012/03/zfa-rudisheni-hadhi-ya-soka-la-zanzibar.html .

Kutokana na jitihada hizo za Awali za kikao hicho cha Serikali na Viongozi na wakuu mbalimbali wa soka Zanzibar hio inatoa mwanga mzuri kwa soka ya Zanzibar kwa kipindi kifupi kama Wataalamu wote wataondoa tofauti zao ndogo zilizopo sasa na kuifanyia ukarabati sera ya uendeshaji wa soka nchini ili kuweza kuleta ushindani mpya na mafanikio makubwa.

Hii ni mara ya kwanza kwa Serikali ya Zanzibar kutamka hadharani azma yake ya kutaka soka nchini lifufuliwe na kuleta hadhi upya kama ilivyokuwa hapo zamani,hivyo kuonyesha muangaza mzuri kati ya serikali na vyama vya michezo nchini kuwa karibu sana tofauti na miaka yote hapo nyuma.

Ikiongea na mdau Holland webblog hii ya ORANJE FOOTBALL ACADAMEY inayofanyia kazi zake nchini humo kwa taarifa mbalimbali za maendeleo ya soka kwa ujumla iliongea na mdau ambae ana haya ya kuelezea kuhusu maendeleo ya soka ya Zanzibar yanawezekana kama itakuwa hivi:

1)Kwanza kabisa ni kuwahamasisha upya wawekezaji/wadhamini/wafadhili katika vilabu kama ilivyokuwa hapo zamani kwani wao ndio wanaosababisha timu kuwa na mpangilio mzuri kimashindano na wachezaji wake kuwa na kazi moja tu yaani kufanya vizuri katika mashindano hayo na hii inapelekea kurejesha imani wa wapenzi na mashabiki kwa kila wanachokishabikia.

2)Kutokana na wakati wa nyuma wafadhili kama akina Naushad Mohammed,Raza,Abdul Satar,SalimTurky, na wengineo walikuwa wakifanya ufadhili kwaajili ya mapenzi yao ya vile vilabu au katika miji yao,hivi sasa soka imebadilika kuwa ni biashara kubwa duniani.

Hivyo ni nafasi nzuri kwa ndugu zetu wafadhili kuweza kuwekeza na kuweza kufanya vizuri zaidi kulikoni wakati ule walipokuwa wakitoa tu bila kuingiza faida yoyote katika soka ingawaje walikuwa wakiifanya michuano kuwa migumu na ya kusisimua kwa msimu mzima kutoka timu hizo kuwa imara na kiushindani tofauti na sasa.

Serikali/vyama vya soka na vilabu kwa ujumla vitafute uwezekano wa kuweza kuwaomba wafadhili wa zamani,na wapya au wafadhili kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza katika soka nchini  ili kuweza kufufua upya ari ya soka na soko la soka nchini.

Zanzibar ni nchi iliyo na vipaji vikubwa sana katika soka ki skills katika ukanda wa afrika mashariki na kati,kwani imeonekana mara nyingi jinsi gani timu ya Taifa ya Zanzibar inavyo tandaza soka katika michuano ya Challenge mbali na kuwa na matatizo kadhaa ya uandaaji na ufadhili wa timu hio.

Ukichukulia nchi kama Holland ni nchi ndogo sana kulinganisha mataifa mengi yanayotamba duniani kisoka,
lakini kutokana na upangiliaji mzuri wa mfumo wake wa timu za watoto inaifanya nchi hio kisoka kuonekana ni taifa kubwa kuliko mataifa karibu yote duniani.

Holland ni nchi inayotoa vipaji zaidi kwa wachezaji vijana kulinganisha na mataifa mengi,na wanaofuatilia mashindano primier league ya holland inaifanya nchi hio kuwa nchi ya pili baada ya spain kuwa na vijana wenye skills nzuri kulinganisha na nchi nyingine za bara la ulaya.

pamoja na kuonekama michuano hio wachezaji wake hawana nguvu.mashabiki wake sio kama england au germany,lakini mchezaji yoyote anaepata elimu ya soka nchini holland anakuwa ni mchezaji anaeweza kuwika katika timu yoyote duniani tofauti ya mchezaji wa england huwezi kumuona anacheza ujerumani,wala wa ujerumani kumuaona anawika nchini spain au italia,wakati yosso wa holland wanatamba nchi yoyote wanapokwenda kuchezea.

Hivyo vipaji kwa watoto kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati vipo nchini Zanzibar kama vitaweza kufatiliwa na kupatiwa wataalamu kuweza kufufua soka nchini.vipaji hivyo vinaonekana kila pembe barani ulaya kwa vijana kutoka zanzibar kungára katika kila klabu wanayochezea ambao hata hivyo bado hawakupata nafasi siku moja kurejea nyumbani kuiwakilisha nchi yao katika michuano mikubwa.

Kama wawekezaji  kila timu itaombwa aidha kujitafutia timu marafiki nje au soko la kuuza wachezaji nje basi itaweza kuwasaidia sio tu wawekezaji bali pia itaweza kuwanufaisha wachezaji kujituma zaidi kwa kila mmoja kuhakikisha anaipata nafasi hio,na hili serikali inaweza kama itaamua kuwatafutia nchi za kufanya hivyo kupitia kwa ambassy zetu mbalimbali zilizoko nje pamoja na nchi marafiki wa Zanzibar.

Aidha wafadhili wangene wanaweza kubuni biashara kwa Watalii kwa kuweka kitega uchumi kitakacho wavutia watalii nchini hivyo kuipatia kipato timu hio kupitia kwa miradi hio.

Alizidi kuongea mdau huyo kwa kusema,pale zamani soka ilikuwa ni ya mapenzi,hivi sasa soka ni biashara kubwa kuliko biashara ya kufuga kuku kama ambavyo baadhi ya wawekezaji wanavyodhania.
kama utakuwa na utaratibu na ufuatiliaji mzuri kwa kuwekeza katika soka vijana wenye vipaji vya vya uhakika na kufatilia soko la kuwauza nchi sehemu yoyote mchezaji mzuri anahitajika na ataendelea kuhitajika kwa bei kubwa kila leo,unadhani unatakiwa uuze kuku wangapi kwa muda gani ili uweke kupata faida sawa na kumuuza mchezaji mmoja tu nje?aliuliza mdau huyo.

Nadhani kwa vile sasa serikali yenyewe imeamua kulitaka hili suala kwa dhati kabisa,basi hii ni nafasi kubwa kwa wawekezaji na viongozi wa soka kuweza kuitumia kufufua soka nchini.viongozi wa serikali tayari wameona soka ni biashara na ni ajira kwa vijana wengi,ambapo nchi kama brasili inaingiza billions za dola kila mwaka kutokana na umati mkubwa wa wachezaji nje ya nchi ya wanaopeleka mishahara yao kufanyia kazi nchini humo,na faida hio sio tu kwa familia zao,bali huajimi mamilioni ya raia wa nchi hio kutokana na miradi mbalimbali ya nyota wake wanayoiendesha nchini humo na wafanyakazi wa miradi hio pia huwaokoa mamilioni ya watu wa familia zao.

3)Alisema zaidi hivi sasa ni kubuni mbinu mpya zitakazo changamsha mashindano hayo na kuleta faida kwa taifa zima kwa ujumla.aidha kuweza kupendekea maoni kwa wadau wa soka nchini na kuangalia ni maoni gani yanafaa ili kuweza kuisaidia ZFA na BMZ kuweza kuongeza au kupungua kitu ambacho labda kinaweza kusaidia zaidi uimara wa uendeshaji mzima wa michuano hio,kwani wale waliotunga sheria ni binadamu na hawa watakao toa mapendekezo yao pia ni binadamu,labda kuna kipengele cha mdau yoyote ukiongezea na kipengele cha zamani unaweza ukapata kitu cha uhakika na kinachohitajika katika soka ya kileo.nani anajua alisema mdau huyo.

4)Kwa mfano timu zinazomiliki michuano ya ligi daraja la kwanza kwa unguja na pemba na timu za mjini tu.kwanini?mashamba au mikoa mingine hakuna timu?nadhani kama timu za mikoani hazina ushindani kuweza kukabiliana na timu za mjini,basi kuundwe kila mkoa kuwe na timu moja kali ya mkoa mzima ambapo watakuwa wakijichukulia wachezaji wao scouting kutoka katika timu zao madaraja ya chini pamoja na timu za watoto za mkoa wao huo.

Hivyo itaifanya timu hio kupendwa na watu wa mkoa mzima hivyo kuleta mtazamo mpya kama vile timu kutoka LONDON,MANCHESTER,LIVERPOOL pamoja na miji mingine hivyo kutapelekea hata raia wa miji hio kutoa michango yao kwa timu za mikoa yao huku wakiongozwa na wabunge na wawakilishi na viongozi wakuu wa mikoa hio hivyo kuifanya ligi ya soka ya Zanzibar kuwa na sura mpya kwa mtazamo kamo huo na hata kwa timu za madaraja ya chini kushindana kama hivyo itaifanya Zanzibar kuwa na ligi ya kuvutia na kushangiliwa na watu hata wasiopenda soka kwani watakuwa wengine wanataka mkoa wao kuona unafanya vizuri hata kama hawajui nini kinaendelea katika soka.

5)Kwa mfano kwa zile timu za miji ambazo zipo katika jimbo moja,mara nyingi kwa soka yetu hivi sasa inavyokwenda ni kuwa inajenga chuki,na sio inajenga uhasama,kuna chuki na uhasama nadhani kiswahili hapa kinafahamika vizuri,michezo ni urafiki,na sio chuki,uhasama ndio unaohitajika kila serehu kama unataka kuendeleza michuano yoyote,hii inapelekea maendeleo katika michuano yoyote.
Timu za mijini zilizo katika majimbo moja aidha vyama vya soka vilazimishe ili klabu iweze kupata usajili wake basi ni lazima iwe na vilabu si chini ya 4 chini yake vya umri mbalimbali.

Na kama klabu itakuwa haina uwezo huo basi vilabu viwili vikubwa jimboni hapo na viwili vya madaraja ya vhini viungane ili kuengeza nguvu moja ya nguvu sana katika jimbo hilo ili kuweza kuweka mashabiki wote wa jimbo zima katika kitu kimoja kutetea jimbo lao,na sio kutengana kuwa chuku jimboni hapo,kwani hata kama kutakuwa na timu 10 jimbo moja,lakini kila timu ina ina wapenzi wawili wa timu yao,utakuwa kiwanjani kuwa wapenzi 4 hivyo kunakuwa hakuna faida yoyota kisoka.

Kama soka inabidi ifufuke basi ifufuke kijimbo,na timu za mikoani kimikoa ikiongozwa na wabunge na wawakilishi na viongozi wakuu wa sehemu zao,kwa mfano alisema mdau huyo.

6)Mwisho alimalizia kwa kusema kuwa, pale zamani Zanzibar ilikuwa ikisubiri timu moja ya klabu yoyote kutwaa ubingwa au ushindi wa pili wa Tanzania kuweza kushiriki michuano ya klabu Bingwa na Washindi wa pili wa Afrika, hivi sasa nafasi zote mbili zipo wazi kwa vilabu viwili vya Zanzibar kushiriki michuano hio.

Ukishinda kuna kiasi fulani kutoka Caf na unapoingia hatua ya makundi kuna Fungu zaidi inapewa kutoka Caf,hivyo nafasi mbali hizi zamani ilikuwa sio rahisi kupatikana kuliko sasa,nadhani hivi sasa ni wakati mzuri kwa wale wafadhili wa zamani kurudi na wapya kuanza kufanya vitu vya uhakika katika soka ambapo kutatoa ajira na faida kubwa kubwa nchini.

7)Michuano kama ZFA FA cup inahitajika ianzishwe ili kuwe kuleta ushindani katika soka kwa vilabu vya madajara mbalimbali kuanzia timu za central league ambapo zitakuwa zikicheza wenyewe kwa wenyewe hadi kupatikana washindi wawili wa mwisho,ambapo watachuana aidha na washindi wawili wa daraja la juu yao ili kutoa washindi wawili watakao iwakaoingia na washindi wawili wa nusu fainali dhidi ya timu za primier league ambao watakuwa nao wakitoana wenyewe na kubakia timu mbili zitakazocheza fainali.

Bingwa wa Michauno hii anaweza kupewe nafasi ya kucheza michuano ya Cecafa Challenge Cup hivyo kuipa kila timu nafasi ya kuchuze michuano hio kuanzia timu za Central league kama zitakuwa na uwezo wa kisoka za kuzichapa vilabu vya madaraja ya juu.hivyo kuifanya michuano ya ZFA FA kuwa ya aina yake na kuviimarisha vilabu vyote nchini kuweza kushinda michuano hio.

Mabingwa wa Zanzibar na washindi wapili watashiriki michuano ya mikubwa ya Afrika ambayo itatosha kwao kujipanga vizuri nayo huku wakiitumia michuano ya Sherehe za Mapinduzi kuwa kama mazoezi ya mayaraisho yao ya michuano hio.

Sio tu kipato bali hata kutaweza kuwafanya vijana na watu wengi kurejea kuviona vilabu vyao vikipepetana kila wiki na kuondoa vijana hao kubakia mabarazani bila cha kufanya na kupelekea kuanza ubunifu wa maovu na utumiaji wa madawa ambayo ni uharibifu mkubwa kwa jamii,kwani hata kama mtoto wako au mdogo wako hayupo katika mambo hayo lakini yule aliekaribu na mtoto wako au jirani yako anaweza akabadisha sura nzima ya maisha yako kuwa katika mtazamo mwingine.

Au vingine nadhani wadau wengi wanaweza kutoa baadhi ya mapendekezo ambayo yanafaa kuweza kufufua soka nchini.
MUNGU IBARIKI ZANZIBAR.alimalizia kwa kusema mdau huyo.