WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday 3 March 2012

YANGA YATOLEWA ORANGE CHAMPIONS LEAGUE

Mabingwa wa soka wa Tanzania Yanga kwa mara nyingine hadithi ni ileile ya kawaida imetupwa nje ya michuano ya Caf Orange Champions League 2012 baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Zamalek pambano lililofanyika katika uwanja wa Jeshi jijini Cairo Misri.
Bao lililotosha kuwasukuma mbele Zamalek kuendelea na michuano hio lilifungwa na Mido katika dakika ya 31 baada ya uzembe wa mabeki wa Yanga kuokoa mpira kizembe na kumwacha Mido akiwa pekeyake na kupiga kichwa kilichokwenda moja kwa moja pembeni kulia na kuandika bao pekee kwa wenyeji hao, kwa ushindi huo Zamelek imeitoa Yanga katika michuano hio kwa jumla ya mabao 2-1.

Katika pambano jingine la michuano hio BejaĆ­a ya Algeria imesonga mbele baada ya kuifunga  3-1 Foullah Edifice ya Chad katika pambano la awali matokeo yalikuwa 0-0.

FC Platiniums Zimbabwe 4-0 Green Mamba FC Swaziland,katika pambano la awali matokeo yalikuwa ni  4-2.Platiniums imesonga mbele kwa kushinda  8-2 baada ya mechi zote 2.
                                      (Mshambuliji wa Zamalek Mido akipachika bao la kichwa).

(Mtaalamu wa O.F.A anaomba muangalie hili bao lilipotokea,beki ambae anachezea katika timu ya taifa ya Stars jinsi ukosefu wa utaalamu kama mchezaji wa kimataifa alivyotoa bao.kama ni mchezaji wa taifa basi huwezi kuokoa mpira kwa kubahatisha kupiga nyuma ya mgongo wako huku huna uhakika nani atatokea.

ara nyingi mpinzani ndie anaechukua mpira na kama upo karibu na goli lako basi hio ndio malipo yako ya kutoa bao la timu pinzani.mipira kama hio ni lazima urejeshe kwa mwenzako alie mbele yako ambae atakuwa anaona mtazamo mzima wa mbele yake kwa wachezaji wote na kama hakuna nafasi ya kumpa pasi mwenzako basi toa mpira kuwa kona au wa kurushwa itategemea nafasi ya uhakika wa mchezaji ambae itamrahisishia kuifanya zaidi kwa urahisi bila kuleta madhara.

Kutokana na utaalamu wetu huyu mchezaji hapo tayari amefeli,kama ni mchezaji wa timu ya Taifa basi makosa kama hayo ndio yanayoirejesha nyuma  Taifa stars na kutofanya vizuri kwa  kuwa na wachezaji wasiokuwa na utaalamu.

Mchezaji aliepata mafunzo tokea akiwa kinda hawezi kupiga mpira wa kuokoa kama huo hata siku moj,inawezekana mara nyingi uzembe kama wa beki wa kati hapo kumsahau Mido akiwa pekeyake kitendo ambacho ni kosa pia,lakini makosa ya kukaba mshambuliaji yanatokea mara nyingi katika kila mechi,lakini uzembe wa kuokoa mpira bila ya kuwa na mafunzo ya tokea Yosso hayo ndio malipo kwa timu hata ya Taifa ya stars).
HILO NI SOMO LETU LA LEO KWA WACHEZAJI CHIPUKIZI KUSOMA NI JINSI GANI MLINZI ANATAKIWA AFANYE.KOSA MOJA LA BEKI SIO SAWA NA MAKOSA 10 YA MSHAMBULIAJI,MLINZI HATAKIWI KUFANYA MAKOSA YA KIZEMBE KAMA KUPIGA CHENGA NYUMBA AU KAMA KOSA LA HUYO MLINZI HAPO JUU KATIKA VIDEO.


MATOKEO MENGINE YA MECHI YA MABINGWA WA AFRIKA NI KAMA HIVI:
ASO Chlef ya Algeria 4-1 ASFA-Yennega  Burkina Faso,katika pambano la awali matokeo yalikuwa ni  0-0. ASO Chlef  inaendelea na michuano hio kwa ushindi wa  4-1.

Missile (Gabon) 3-2 Africa Sport
Africa Sport (Ivory Coast) 2-0 Missile
Africa Sport imesonga mbele kwa jumla ya mabao 4-3.

Tusker (Kenya) 0-0 APR
APR (Rwanda) 1-0 Tusker
APR imesonga mbele kwa ushindi kiduchu wa 1-0 baada ya kutoka sare ya 0-0 katika pambano la awali.

Coin Noir Mitsamiouli (Comoros) 1-0 Ethiopian Coffee
Ethiopian Coffee (Ethiopia) 4-1 Mitsamiouli
Ethiopian Coffee imesonga mbele kwa  4-2.


URA (Uganda) 3-0 Lesotho Correctional Services
Lesotho Correctional Services (Lesotho) 0-0 URA
URA imetinga hatua ya pili  kwa  3-0.


Brikama (Gambia) 0-1 US Ouakam
US Ouakam (Senegal) 0-1 Brikama
Brikama imesonga mbele kwa  2-0.


Sony de Ela Nguema (Eq. Guinea) 0-3 Dolphins
Dolphins (Nigeria) 3-0 Sony de Ela Nguema
Dolphins imetinga hatua ya kwanza 6-0.


LISCR (Liberia) 0-2 Berekum Chelsea
Berekum Chelsea (Ghana) 3-0 LISCR
Berekum Chelsea imesonga mbele kwa  5-0.

Green Mamba (Swaziland) 2-4 Platinum
Platinum (Zimbabwe) 4-0 Green Mamba
Platinum imetinga hatua ya pili  kwa ushindi mnono wa 8-2.

Japan Actual (Madagascar) 5-1 Power Dynamos
Power Dynamos (Zambia) 3-0 Japan Actual
Power Dynamos imesonga mbele kwa idadi kubwa ya mabao 8-1.