WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Wednesday 18 April 2012

MAXIMO ASHAURI KUUNDWA KWA TIMU ZA TAIFA ZA WATOTO NCHINI

Anna Nkinda,  Brazil
KLABU za soka nchini zimeshauriwa kuwekeza kwenye timu za vijana na watoto wenye umri kuanzia miaka nane ili kuja kupata timu bora ya taifa miaka ya mbele.

Wito huo umetolewa jana na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Taifa Star, Marcio Maximo wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Sao Paul.

Maximo alisema kuwa timu nyingi ambazo ni bora na zinafanya vizuri kwenye mashindano kutokana na kuwaandaa mapema na muda mrefu watoto wenye vipaji vya mchezo huo ambao ndio wanaotunzwa na kupandishwa hadi kufikia katika timu kubwa ya Taifa ya nchi au timu kubwa za vilabu.

Kuhusiana na uvumi ulioenea kuwa anataka  kwenda kufundisha timu za Taifa Stars, Azam au Yanga alisema hakuna ukweli kwenye taarifa hizo kwani kwa sasa ana mkataba wa kufundisha timu ya Democrata.
“Timu ya Taifa Star ina kocha mzuri ambaye namuheshimu na kukubali ufundishaji. Nina imani kupitia kocha huyo Watanzania watazidi kuendelea katika soka na kufika mbali zaidi”, alisema.

Mwalimu huyo wa zamani wa Taifa Stars alisema bado ana mawasiliano mazuri na Watanzania na anajivunia na kujisikia kama Tanzania ni nchi yake ya pili.

Hata hivyo pamoja na kauli hiyo ya Maximo, tangu kuwasilia kwa Kocha Jan Poulsen, Tanzania imeendelea kuporomoka viwango kila mwezi, ambapo sasa inashika nafasi ya 145 kwa mujibu wa orodha ya viwango vya ubora iliyotolewa na Shirikisho la Soka Ulimwenguni (Fifa) mwezi huu.