WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Sunday 22 April 2012

NGORONGORO HEROES YAANZA VIZURI

TIMU ya soka ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu raundi inayofuata ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana baada ya kuichapa Sudan mabao 3-1.

Ngorongoro iliumudu mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa asilimia kubwa huku wachezaji wake wakionesha staili mbalimbali za kuumiliki mpira na kujaribu kufunga mabao.

Thomas Ulimwengu alifungua pazia la mabao kwa timu hiyo baada ya kufunga katika dakika ya 15 kwa kumalizia krosi safi iliyopigwa na Simon Msuva. Mchezaji Ramadhani Singano alifunga bao la pili baada ya kupewa pasi na Ulimwengu kabla ya kuumalizia nyavuni katika dakika ya 20.

Baada ya kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0, Ngorongoro ilianza kipindi cha pili kwa kasi na kulishambulia lango la Sudan. Mchezaji Simon Msuva aliiongezea Ngorongoro Heroes goli la tatu kwa kichwa dakika ya 69 baada ya kuunganisha mpira wa kona.

Sudan ilipata bao lake dakika ya 89 kupitia kwa mchezaji Sharafeldin Shaiboub.

MATOKEO MENGINE YA MICHUANO HIO NI KAMA HIVI IFUATAVYO:

Tanzania  - Sudan 3-1

Morocco - Mauritania 5-0

Namibia - Rwanda 0-2

Uganda - Mozambique 4-0

Zimbabwe  -  Botswana  4-0