WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Monday, 23 April 2012

O.F.A YATOA PONGEZI KWA MH WAZIRI WA HABARI,UTAMADUNI,UTALII NA MICHEZO

Kituo cha kukusa soka kwa vijana nchini  ORANJE FOOTBALL ACADEMY kinatoa pongezi zake za dhati kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na MICHEZO Mh Said Ali Mbarouk kwa juhudi zake za makusudi za kiutendaji katika upande wa michezo.katika hatua yake ya kuanza kufuatilia mwenyewe shuhuli muhimu za maendeleo ya michezo na kuanza kutoa visomo vya manufaa na vyenye kuonyesha mwamko wa kuleta mapinduzi na maendeleo ya soka nchini Zanzibar.

Katika taarifa yake aliyoitoa katika uzinduzi wa michuano ya vijana ya jimbo la Magogoni "JIHADI CUP" michuano ambayo imeanzishwa na mwakilishi wa jimbo hilo Mh Abdillah Jihadi kwa lengo la kuibua vipaji jimboni humo  ambapo Mh Waziri amewataka Wadau wote nchini kuanza kufungua ukurasa mpya wa kujenga ushirikiano na Vyombo  vya soka vya  Zanzibar BTMZ na ZFA ili kuweza kuleta maendeleo nchini ili kukipa nafasi chama hicho kuanza Upya kujenga mikakati ya Kuleta Maendeleo ya soka ya Zanzibar kwa kipindi kifupi kijacho.

Pamoja na hatua yake hio pia Mh Waziri wa Michezo aliwataka wadau wote wenye mawazo mazuri  ambayo wanaona yataweza kuisaidia Zanzibar katika kufikia hatua nzuri katika soka watoe maoni yao kwa vyombo vinavyohisika na michezo Zanzibar ila tu aliwataka wadau hao kufuata sheria na kanuni za Nchi.

Pia Mh Waziri Said Ali Mbarouk alivitaka vilabu nchini kuviunga mkono vyombo  hivyo vya soka  na vinginevyo vyombo vya soka vya Zanzibar pia kushirikiana kikamilifu na vilabu na kufanya ushirikiano wa wadau wote kuanzia ngazi za Vilabu hadi Serikali.

Mbali na kituo kutoa shukurani kwa Mh Waziri wa Michezo Said Ali Mbarouk pia kituo chetu cha kukuza soka kwa vijana ORANJE FOOTBALL ACADEMY kinatoa pongezi kwa Mwakilishi wa Magogoni Mh Abdillah Jihadi kwa kujitokeza kuwa mfano wa kwanza katika safu ya viongozi wa Zanzibar kuonyesha kile ambacho Mh Rais na Makamo wa pili wa  Rais pamoja na Waziri wa Michezo wamekuwa wakikitilia mkazo mkubwa wa" kufufua soka ya Zanzibar".

Kituo chetu cha kukuza soka kwa vijana pia kinawaomba Wawakilishi na Wabunge wa UNGUJA NA PEMBA  kuanzisha mashindano kama hayo katika majimbo ya ili kwenda sambamba nchi nzima kuwa na mashindano kama hayo kwa muda ambao utakuwa umepangwa na vyombo vya soka vya Zanzibar ilikuweza kuifanya michuano hio kuwa ya kitaifa na ikiwezekana mabingwa wa michuano hio ya vijana wapambanishwe ili kuweza kumpata bingwa wa jimbo bora la Zanzibar ambapo michuano hio itakuwa ni kama mfano FA ya vijana wa Zanzibar.

Katika Hatua njingine Oranje Football Academy inatoa pongezi zake za dhati kwa chama cha soka cha ZFA kwa kuwataka vijana wanaoshiriki michuano hio kujituma na kuonyesha uwezo wao kwani makocha watapita na kufatilia michuano hio na kuweza kupata wachezaji wa timu za Taifa za U15, U17 na U20 ambao ndio watakajenga timu hizo na kuendelezwa kama nchi zote duniani zinavyofanya.

Hii ni moja ya hatua kubwa ambayo haijawahi kutokea hapo nyuma kwa viongozi wa juu wa ZFA kutilia mkazo suala la timu za Taifa za chipukizi kutoka miaka 15.

kutoka na majimbo yote ya Zanzibar kusheheni chipukizi wenye vipaji vikubwa hivi sasa ni wakati mzuri kwa Wabunge na Wawakilishi wa majimbo yote ya Zanzibar kuiga mfano wa Mh Abdillah Jihad ili kwenda sambamba na michuano hio kuwapata vijana nchini nzima kama wanavyofanya wenzetu kukusanya vipaji hata kama ni 100 au zaidi na kuwapatia mchujo hadi kufikia idadi ya kuwa na nyota bora wa Taifa kwa kila rika ambao ndio maendeleo yanayotakiwa kwa muda mfupi ujao.

Timu zinazoshiriki michuano ya Jihad Cup ni
New Africa,Eleven Fighters ,University,
Taifa Jipya,Sayari Fc,Danger Boys,
Grenada,Maisara Fc,na Super Eagle.