WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Sunday 21 April 2013

CECAFA BADILIKENI

WADAU WA SOKA MBALIMBALI WANAOISHI NJE YA NCHI WAMETOA MAWAZO YANAYOFANA KWA KUUTAKA UONGOZI WA SOKA KATIKA NCHI ZA AFRICA MASHARIKI NA KATI "CECAFA" KUBADILIKA NA KUWACHANA NA MWENENDO WAO WA KIZAMANI WA KUENDESHA MASHINDANO HAYO.

TOKEA KUANZISHWA KWA SHIRIKISHO HILO KILA MWAKA MASHINDANO HUA YANAFANYIKA KATIKA NCHI MOJA NA KUPANGWA MAKUNDI HADI KUMPATA BINGWA WAKE. NA HIO HAIONEKANI KUISAIDIA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWANI TIMU ZAO NCHI HIZO NDIO SEHEMU ILIYOKUWA CHINI KULIKO ZOTE KISOKA KATIKA BARA ZIMA LA AFRICA.MBALI NA KUWA MASHINDANO HAYO NDIO TEGEMEO PEKEE LA KUKUZA SOKA KWA NCHI HIZO PAMOJA NA YALE YA TIMU ZA TAIFA YA NCHI HIZO.

WADAU HAO WAMEUOMBA UONGOZI WA SOKA NCHINI "TFF" KUONGEA NA WADAU WENZAO KUANZISHWA MPANGO MPYA WA KUYAENDESHA MASHINDANO HAYO AMBAPO YATAWEZA KUNYANYUA MAENDELEO YA SOKA KATIKA UKANDA HUO.

WADAU HAO WALISEMA NI "UNFAIR" KUONA TIMU NYINGI KATIKA LIGI KUU ZA NCHI HIZO ZINAJITAHIDI NA MWISHO WAKE MSHINDI WA TATU,WANNE HADI WA TANO HAPATI MANUFAA YOYOTE, WANAONUFAIKA NI MSHINDI WA KWANZA NA WAPILI AMBAO MAISHA WANAKUWA NI SIMBA NA YANGA NA HIVI SASA INAONEKANA AZAM KUJIPENYEZA KATIKA NAFASI HIZO MBILI ZA JUU.

HIO NI KUONYESHA TIMU KAMA KAGERA SUGAR,MTIBWA SUGAR NA NYINGINEZO MAISHA KAZI YAO ITAKUWA ZINASHIRIKI TU LIGI KUU NA KAMWE ZISITEGEMEE KUTWAA UBINGWA HIVYO TIMU HIZO MAISHA HAZITOIWAKILISHA NCHI KIMATAIFA HATA KATIKA UKANDA HUU WA AFRICA MASHARIKI NA KATI.

IMEFIKIA MUDA SASA "CECAFA  IBADILIKE KIAKILI" WALIONGEZA WADAU HAO

"CECAFA" IANZISHENI MASHINDAO AMBAPO HADI MSHINDI WA TANO KATIKA LIGI AINGIE KATIKA MASHINDANO YA KLABU BINGWA ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI, NA WACHENI "UPUNGUFU WENU WA AKILI" WA KUZIALIKA TIMU ZA ZAMBIA,IVORY COAST NA NYINGINEZO KUJA KUSHIRIKI MASHINDANO YETU,
 "MBONA WAO HAWATUALIKI MASHINDANO YAO" TENGENEZENI MFUMO MPYA, WALISEMA WADAU HAO.

MSHINDI WA KWANZA AMBAE NI BINGWA HADI MSHINDI WA TATU WASHIRIKI MOJA KWA MOJA FAINALI HIZO,

MSHINDI WA NNE NA WA TANO WASHIRIKI MASHINDANO HAYO KWA NJIA YA MTOANO YA NYUMBANI NA UGENINI HATI KUPATIKANA IDADI YA TIMU ZITAKAZOWEZA KUUNGANA NA WALE WASHINDI WATATU WA FAINALI HIZO.

KATIKA KUPATA IDADI HIO BILA SHAKA TIMU ZITAKUWA NYINGI SANA NA MASHINDANO KUWA NI MAREFU, HILO SIO TATIZO ILA TUTATOA PICHA MPYA YA MASHINDANO NI KUZIGAWA TIMU HIZO KWA MAKUNDI  MATATU HADI MANNE.

KILA KUNDI LITAKUWA KATIKA NCHI MOJA AMBAPO MASHINDANO HAYO YATAFANYIKA KWA WAKATI MMOJA KATI YA NCHI TATU HADI NNE NA KUOMBA MASHIRIKA KURUSHA LIVE MASHINDANO ILI WADAU WA NCHI ZOTE WAWEZE KUFATILIA MECHI ZOTE MOJA KWA MOJA,NA HII ITASAIDIA MSISIMKO WA MASHINDANO PIA MAPATO KUONGEZEKA YA MILANGONI KULIKONI KUFANYIKA NCHI MOJA.

WASHINDI WAWILI AU WATATU WA KILA KUNDI NDIO WATAKAOINGIA MOJA KWA MOJA KATIKA FAINALI ZA MASHINDANO KWA MFUMO TULIOKUWANAO SASA ILI KUMPATA BINGWA BINGWA HUYO.

KWA MFANO HUO TIMU KAMA KAGERA SUGAR,MTIBWA SUGAR NA HATA KATIKA NAFASI YA NNE NA YA TANO WANAWEZA PIA KUINGIZWA MABINGWA WA KOMBE LA MTOANO  "FA CUP" ILI WASHIRIKI KATIKA MASHINDANO HAYO AMBAPO TIMU HADI ZA DARAJA LA PILI ZITASHIRIKISHA NA KUWANIA NAFASI HIO YA KUCHEZA NA TIMU ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI,

 HIVYO MASHINDANO YOTE NCHINI YATAKUWA NA MFUTANO NA MSISIMKO WA HALI YA JUU KWA VILE KILA TIMU ITAKUWA NA NAFASI YA KUTWAA MOJA YA NAFASI HIZO.

VINGINEVYO KILA SIKU ITAKUWA TIMU ZENYE HAKI NCHINI NI YANGA NA SIMBA TU.
KWAMAANA HIO TIMU ZA SIMBA NA YANGA NA SASA AZAM NI BORA KUWA NA LIGI YA TIMU HIZO TATU NCHINI NA MABINGWA KUSHIRIKI "CAF" NA "CECAFA" NA TIMU NYINGINE HAZINA HAKI YOYOTE KAMA TIMU NCHINI WALIMALIZIA.

"IMEFIKIA MUDA SASA CECAFA KUAMKA NA KUANZISHA MFUMO MPYA WA MASHINDANO HAYO."