WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday 6 April 2013

MAONI YA "KUKARABATI" SOKA LA VIJANA NCHINI

KITUO CHA KUKUZA SOKA KWA VIJANA NCHINI ORANJE FOOTBALL ACADEMY,
KINATOA USHAURI KWA TFF PAMOJA NA WADAU WOTE KUHUSIANA NA KAULI YA VIONGOZI WA  TFF YA KUTAKA KULIJENGA SOKA LA VIJANA NCHINI KAMA IFUATAVYO:

KAMA TUKITAKA KUENDELEA KISOKA KWANZA TUANGALIE JINA LA NCHI KAMA
" IVORY COAST ? " MOJA KWA MOJA MACHO NA MASIKIO AU HISIA ZA KILA MTU ZITAKWENDA MOJA KWA MOJA "DROGBA" AU "YAYA TOURE" "KALU" NA WENGINEO.

HIO NI KUMAANISHA SOKA INATOA MABALOZI WA NCHI WA KUWEZA KUIFANYA NCHI KUTAMBULIKANA  KIMATAIFA,
HIVYO TUNAOMBA KWANZA SOKA LA VIJANA NCHINI  " LIRUHUSIWE VILABU VYOTE VYA PRIMIER LEAGUE"
WARUHUSIWE MOJA KWA MOJA WACHEZAJI WAO WOTE WA TIMU ZAO "B" "C" KUTUMIKA MOJA KWA MOJA KATIKA KIKOSI CHA KWANZA CHA TIMU HIZO WAKATI WOWOTE PALE KOCHA ATAKAVYOAMUA KUWATUMIA NYOTA HAO.

LENGO NI KUWAKOMAZA NA KUWAPA NAFASI KWA KILA MCHEZAJI ATAKAEJITUMA IPASAVYO NA KUONYESHA KIWANGO CHA KURIDHISHA HAPO CHINI KUITWA MOJA KWA MOJA KATIKA KIKOSI CHA KWANZA KATIKA MECHI ZA LIGI AU MTOANO, NA HII ITALETA USHINDANI KWA VIJANA WOTE KUWANIA NAFASI HIZO ZA KUCHEZA WAKATI WOTE WAKIWA  "FITI" MSIMU MZIMA.

HII ITAIFANYA KLABU KUNUFAIKA NA TAIFA KUFAIDIKA NA VIJANA KULIKONI HIVI SASA KUWASAJILI WACHEZAJI "KIDUCHU" KUTOKA TIMU "B" AMBAO PIA HUWA HAWATUMIKI IPASAVYO KWAVILE KLABU INASAJILI NA KUPOTEZA GHARAMA NYINGI KUSAJILI WACHEZAJI KUTOKA NDANI NA NJE YA NCHI AMBAO PENGINE KIWANGO NI SAWA AU CHINI YA VIJANA HAO.

KAMA KLABU ZIKIRUHUSIWA MUDA WA KUSAJILI KATIKA LIGI KUU "BASI USAJILI HUO UENDANE NA USAJILI WA TIMU ZAO "B" "C" AMBAO VIJANA HAO WATAWEZA KUZITUMIAKIA TIMU ZAO KUBWA WAKATI WOWOTE WAKIHITAJIAKA

HIVYO IENDANE SAMBAMBA NA TIMU ZA DARAJA LA KWANZA HADI MADARAJA YOTE "KURUHUSIWA VIJANA WAO WA TIMU NDOGO KUTUMIKIA USAJILI WA TIMU KUBWA MOJA KWA MOJA KAMA AMBAVYO NCHI ZOTE ZILIZOENDELEA KISOKA ZINAFANYA HIVYO"

"TUSIWE KICHWA NGUMU" KILA SIKU KUTEGEMEA USAJILI MPYA "SURA MPYA" GHARAMA ZISIZOKUWA ZA LAZIMA WALA MAANA YOYOTE ILE KAMA VIJANA WATAKUWA WANAO UWEZO WA KUZIBA MAPENGO KATIKA TIMU ZAO KUBWA MOJA KWA MOJA ITAKUWA NI BORA KWAO NA KWA TAIFA KWA UJUMLA.

ZAIDI WADHAMINI WA VILABU VIKUBWA NA WAFADHILI WATENGE FUNGU PAMOJA NA SERIKALI KWA PAMOJA " FUNGU HILO LIENDE KATIKA BAJETI YA  VILABU "B" "C"  ILI KILA TIMU IANZE KUVUNA MATUNDA YA VIJANA INAYOWAJENGA WAO WENYEWE NA SIO ZAIDI YA KUTEGEMEA "KILA MWAKA SURA MPYA"

KUNA WACHEZAJI WANAWEZA KUWA WAZURI KATIKA TIMUA ZAO, LAKINI WASIWE "FITI" WALA KUWA NA "TIJA" YOYOTE KATIKA TIMU WANAZOKWENDA, NA HILI NDIO TATIZO KUBWA LA KILA MWAKA KWA SOKA NCHINI.

HIVYO WACHEZAJI WA KUWATENGENEZA KATIKA TIMU NDOGO ZA VILABU MARA ZOTE WANAKUWA WA UHAKIKA KWA VILE UMEWATENGEZA KWA JINSI UNAVYOTAKA WACHEZE KIWANJANI.


ZAIDI VILABU HIVYO TIMU ZAO  NDOGO VIINGIZWE KATIKA LIGI ZA MADARAJA MBALIMBALI ILI ZITOE CHANGAMOTO LA KUPANDISHWA VIWANGO KWA TIMU NYINGINE PAMOJA NA WAO KUJITENGENEZA KIMASHINDANO TAYARI KUZIWAKILISHA TIMU ZAO WAKATI WOWOTE WANAPOHITAJIKA PAMOJA NA TAIFA.

KOMBE LA UHAI CUP LIUNGANISHE NA KOMBE LA COPA COCA COLA ILI KUWAPIMA VIJANA WA COPA COCA COLA UWEZO WAO NA WALE WA UHAI CUP AIDHA KOMBE LA "TAIFA LIREJESHWE KWA TIMU ZA VIJANA ZA MIKOA YOTE NCHINI KUPAMBANISHA PAMOJA NA ZILE ZA UHAI CUP" KULIKONI  KUTUMIA "TAIFA CUP"
KWA WACHEZAJI WALE WALE WA YANGA,SIMBA,AZAM,AMBAO MSIMU MZIMA WANACHEZA LIGI,TIMU ZA TAIFA,HIVYO KUTOTOA NAFASI KWA VIJANA KUONEKANWA NA KUKUZA SOKA NCHINI.

MWISHO TFF IWASHIRIKISHE WADAU WOTE NCHINI KUTOA MAWAZO YAO, JINSI GANI YA KILA MTU ATACHANGIA MAWAZO HAYO KUWEZA KUBORESHA AU "KULIKARABATI " SOKA LA VIJANA NCHINI NA KUWACHANA NA MAWAZO YA TFF PEKEE AMBAO MARA NYINGI YANAONEKANA "KUGONGA UKUTA"

KITUO CHA KUKUZA SOKA KWA VIJANA NCHINI ORANJE FOOTBALL ACADEMY KINAKUACHIENI
WADAU WOTE NCHINI KUENDELEZA "KASI" HII YA MAONI YA "KUKARABATI " SOKA LA VIJANA NCHINI KWA LENGO LA MAENDELEO YA TAIFA. SOKA NI AJIRA NA ITACHANGIA UCHUMI WA NCHINI KATIKA NYANJA ZOTE KAMA KWELI NCHI IKIWA MAKINI.