Vijana wa Oranje Football Academy U17 watashuka dimbani leo Jumamosi 6/4/2013 Saa 2:00 asubuhi katika Kiwanja cha Small Simba wakicheza mchezo wa Mtoano na timu ya New Vision.
U14 wao watashuka dimbani pia leo Jumamosi 6/4/2013 Saa 10:00 jioni katika Kiwanja cha Small Simba wakicheza mchezo wa Ligi Round No. 12 na timu ya Black Selar.
katika mechi zote mbili vijana wa kituo cha O.F.A watashuka viwanjani wakiwa na wachezaji wao wakonge kwa U17 wakiwa na nyota wake akila Bale, Riberry, D Jong, Ed U, Chollow Don .
Huku ndugu zao wa U14 wakishusha kikocha cha akina Kizizu, Gerrad, Anuar, Twenty, D gear, Moh'd (Luis Nani)
Vikosi vyote viko imara tayari kwa mechi hizo mbili na tunategemea ushindi mnono kwa vijana wetu U17 na U14.
O.F.A U17 wao wakiwa tayari wamefuzu na kutinga hatua ya 12 Bora katika kundi C na sasa vijana Uwamemaliza mechi zao za awali na kupata mapumziko ya wiki mbili na kusumbiri ratiba ya mechi za mtoano na fainaliz za 12 Bora.
Chipukizi wa U14 wanaendelea na mechi za makundi na wiki iliyopita waliweza kuifunga timu ya Ivory Coast goli 2 - 1 na kusogea katika nafasi ya tano huku wakiwa wamebakisha michezo mitatu kukamilisha michezo yao kukamilisha ratiba ya ligi hio na kuona matokea ya mechi zote yatakwendaje kuingia katika ya 12 Bora .
Chipukizi hao wanaendelea na mazoezi na vijana wapo katika hali nzuri na ari kubwa.
Kituo cha kukuza vipaji cha Oranje Football Academy mpaka sasa kinaendelea vizuri hasa kwa kuwatayarisha vijana na kuwaweka katika mazingira mazuri ya kucheza mpira na kukuza vipaji vyao.
licha ya kuwa kituo hicho hadi sasa bado hakijatowa wachezaji kuanza kwenda nje katika ukanda huu wa Afrika ya mashariki na Ulaya. Bado tunajivunia kuwa na kituo bora kwa Zanzibar kwa kuweza kuleta wageni kutoka nchi mbali mbali hapa nchini kwa lengo la kuja kuona maendeleo ya vijana wetu.
Kituo cha Oranje Football Academy tayari kimetoa nyota mbalimbali wanaochezea madaraja tofauti hapa Zanzbar kuanzia ligi kuu huku nyota wake wawili Seif Abdalla (Karihe)Ambae ndie alieifungia Azam bao la ushindi pambano la kimataifa kule nchini Liberia na Mudathir wote wanachezea AZAM F.C ya jijini Dar es Salaam ambayo ni moja ya miamba mitatu mikubwa ya soka hapa nchini.
KWA NIABA YA ORANJE FOOTBALL ACADEMY INAWATAKIA AZAM F.C KILA LA KHERI KATIKA PAMBANO LAKE LA MAREJEANO
..........................................
WAKATI HUOHUO KITUO CHA KUKUZA SOKA KWA VIJANA NCHINI ORANJE FOOTBALL ACADEMY KINACHO SHIRIKIANA NA NA KAMPUNI YA AFRISOCCER CONSULTING YA JIJINI DAR ES SALAAM,
KITATOA PONGEZI ZA DHATI KWA UONGOZI WA TFF WA KUAMUA KWA MAKUSUDI KABISA KULETA MAPINDUZI YA SOKA NCHINI KWA KUWATAKA WADAU WOTE NCHINI KUSHIRIKIANA ILI KUIFANIKISHA ADHMA HIO KWA MANUFAA YA TAIFA.
SOKA NI BALOZI WA KIMATAIFA AMBAPO NCHI HUNUFAIKA NA UMAARUFU SIO TU KWA SOKA BALI HUPELEKEA NYANJA ZOTE KUFUNGUKA ZA UCHUMI KUFUNGUKA KAMA SOKA NCHI IKISHIRIKISHA WADAU WOTE KWA UJUMLA NA KUWEZA KUSHIRIKIANA ILI KULETA MAENDELEO HAYO NCHINI.
NI RAHISI KUTANGAZIA UTALII,UCHUMI WA NCHI KUPITIA SOKA KAMA BALOZI WAKE MKUU WA NJE AMBAPO MAFANIKIO YAKE YATAMNUFAISHA KILA MWANANCHI NCHINI HATA KAMA HAHUSIKI AU KUPENDA SOKA.
HII HAPA CHINI NI COPY YA MAELEZO YA TFF.
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezindua rasmi Mpango wa Maendeleo wa Mpira wa Miguu (Technical Development Plan- TDP) wa 2013-2016 ambao pamoja na mambo mengine unahusisha kutazama upya mfumo wa mashindano na kuunda kanda kwa ajili ya kusimamia maendeleo.
Uzinduzi huo ulifanywa jana na Rais wa TFF, Leodegar Tenga katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na washirika mbalimbali wakiwemo wachezaji, viongozi wa mpira wa miguu, Serikali, klabu na Wahariri wa Michezo.
Rais Tenga amesema mpango huo unafuatia ule wa 2004-2007, na 2008-2012 ambayo ilitengenezwa kwa msaada wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). Mpango wa sasa umetengenezwa na TFF kwa kufuata mpango mfano (standard plan) wa FIFA.
Amesema mpango wa sasa ni wa kiufundi zaidi kwa vile umelenga kuendeleza mpira wa miguu, kwani iliyotangulia ilihusisha zaidi kutengeneza muundo wa TFF, kazi ambayo imekamilika kwani sasa shirikisho lina vyombo mbalimbali vya kusimamia mchezo huo.
“Wakati ule tulikuwa na Ligi Kuu tu, lakini tumeongeza mashindano ya aina mbalimbali kama U17, U20, Kombe la Taifa na sasa michuano ya Copa Coca-Cola itakuwa ya U15. Pia tukatengeneza Kanuni za Fedha, kilichomo katika mpango wa sasa ni kujenga mpira. Chombo (TFF) tayari kipo,” amesema.
Rais Tenga amesema TFF imefika hapa kutokana na watu kujitolea ambapo ametaka moyo huo uendelezwe, lakini akasisitiza washirika wote kuwa na mpango huo na kuusoma kwani umetokana na maoni yao ambapo kila mmoja ana kazi ya kufanya katika mpango huo.
“Naomba washirika wote wasome mpango huu. Kama mtu una mawazo zaidi baada ya kusoma, toa maoni yako. Mpango huu si Msahafu, utabadilika kutokana na maoni ya watu. Kama una mawazo zaidi, toa maoni yako kwa lengo la kujenga, isiwe kazi ya kulaumu tu kuwa mpango una upungufu. Mabadiliko yanafanyika kutokana na mawazo mapya,” amesema.
Amesema maendeleo ya mpira wa miguu ni mchakato mrefu, kwa hiyo unahitaji ushiriki wa watu kutokana na ukweli kuwa uongozi wa mpira wa miguu Tanzania bado ni wa kujitolea.
Rais Tenga amesema ahadi ya TFF ni kushirikiana na washirika mbalimbali kuhakikisha kuna maendeleo kwa faida ya mpira wa miguu wenyewe na nchi kwa ujumla.
Amewashukuru wote waliotoa maoni kwa ajili ya mpango huo wenye kurasa 76. Mpango huo ulioandaliwa na Mkufunzi wa FIFA, Henry Tandau, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni na Ofisa Maendeleo wa TFF, Salum