WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Thursday 16 May 2013

BREAKING NEWS: MUDATHIR YAHYA WA O.F.A AITWA STARS KUIVAA MOROCCO

KIM Ataja 26 Stars Wa Kuivaa Morocco
Thursday, 16 May 2013 16:06
KIUNGO MKALI WA ORANJE FOOTBALL ACADEMY MUDATHIR YAHYA AMBAE HIVI SASA YUPO AZAM F.C BILA MALIPO YOYOTE YA SHERIA ZA SOKA DUNIANI FIFA AMEITWA KWA MARA YA KWANZA KUJIUNGA NA TIMU YA SOKA YA TAIFA STARS ITAKAYOKWENDA NCHINI MOROCCO KUPAMBANA NA TIMU HIO LION OF ATLAS SIKU YA TAREHE 8 JUNI PAMBANO LITAKALOPINGWA KATIKA UWANJA WA KISASA WA MJINI MARRAKESH.

MUDATHIR YAHYA KWA KUITWA KWAKE HIVYO AMEWEZA KUMPIGA BAO LA KISIGINO NYOTA WA ORANGE FOOTBALL ACADEMY SEIF ABDALLAH "KARIHE"AMBAO AWALI WOTE WALIITWA KATIKA KIKOSI CHA PILI CHA TAIFA STARS HIVYO KUMWAMBIA "KARIHE"ASUBIRI KIDOGO WITO WA KUJIUNGA NA WAKUBWA HAO WA STARS.

KITUO CHA KUKUZA SOKA KWA VIJANA NCHINI KINATOA PONGEZI KWA KINDA HUYO KUITWA KWAKE KATIKA TIMU YA TAIFA STARS AMBAYO INAWANIA NAFASI YA KUFUZU MASHINDANO MAKUBWA YA SOKA KULIKO YOTE DUNIANI "WORLD CUP".

KITUO CHETU CHA KUKUZA SOKA NCHINI O.F.A KINAMTAKIA KILA LA KHERI NYOTA WAKE HUYO KUWEZA KUITWA KWAKE KATIKA MASHINDANO YENYE HADHI YA HALI YA JUU KIMATAIFA SAWA NA MCHEZAJI WA TIMU YOYOTE DUNIANI WAKAI ANAPOITWA NATIONAL TEAM YA NCHI YAKE KUIWAKILISHA NCHI KATIKA KUWANIA NAFASI YA KUISUKUMA NCHI YAKE KATIKA FAINALI HIZO AMBAZO SAFARI HII ZITAFANYIKA NCHINI BRASIL HAPO MWAKANI.

....................................................................
HIZI HAPA NI HABARI ZAIDI ZA TAARIFA HIZO
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 16 mwaka huu) ametaja kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiwinda kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco.

Katika kikosi hicho, Kim ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao wamewahi kuchezea timu hiyo, huku akiacha wengine watatu aliokuwa nao kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Morocco ambapo Taifa Stars ilishinda mabao 3-1.

Wapya aliowaita katika kikosi hicho kitakachoingia kambini Mei 20 mwaka huu, saa 1 jioni kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam ni Ally Mustafa, Vicent Barnabas, Juma Luzio, Haruna Chanongo, MUDATHIR YAHYA  na Zahoro Pazi. Wachezaji aliowaacha ni Shabani Nditi, Nassoro Masoud Cholo na Issa Rashid.
Kikosi kamili cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho kabla ya kwenda Morocco kitapita jijini Addis Ababa, Ethiopia kucheza mechi ya kirafiki Juni 2 mwaka huu dhidi ya Sudan ni kama ifuatavyo;

Makipa:
Nahodha Juma Kaseja (Simba), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar) na Waziri Salum (Azam).

Viungo:
Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba),MUDATHIR YAHYA (Azam) na Salum Abubakar (Azam).

Washambuliaji:
John Bocco (Azam), Juma Luzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Zahoro Pazi (JKT Ruvu).

Kocha Kim amesema kikosi kitakachoingia kambini kitakuwa na wachezaji 24 ambapo Samata na
Ulimwengu watajiunga na timu jijini Marrakech, lakini wachezaji atakaondoka nao Dar es Salaam kwenda Addis Ababa ni 22 ambapo ataacha kipa mmoja na mchezaji mmoja wa ndani.

Awali TFF ilikuwa imeitafutia Taifa Stars mechi ya kirafiki Juni 1 mwaka huu dhidi ya Algeria, Libya au Misri. Lakini baadaye Algeria ikasema itacheza na Togo, wakati Misri ilitaka mechi hiyo ichezwe Juni 4 jijini Cairo, jambo ambalo lisingewezekana kwa Stars kwani ina mechi ya mashindano Juni 8 mwaka huu.

Kwa upande wa Libya mechi hiyo ilikubaliwa ichezwe Tunis, Tunisia, Juni 2 mwaka huu. Lakini baadaye Libya ikataka mechi hiyo ichezewe jijini Tripoli ambapo TFF ilikataa kutokana na sababu za kiusalama.

chanzo: www.tff.or.com