Kituo cha kukuza soka kwa vijana nchini Oranje Football Academy " O.F.A " kupitia katika blog yake hii pamoja na plus.google.com ambayo inahifadhi picha za matukio mbalimbali ya picha yanayowekwa katika blog hii inayomilikiwa na kituo cha O.F.A hadi kufikia leo imeweza kufikisha idadi ya karibu nusu milioni ya watu duniani kote waliotembelea links hizo bila ya kujumisha idadi hio na official website ya kituo hicho www.ofaznz.net pamoja ya video ya YOTUBE ambavyo vyombo vyote hivyo kwa ujumla itafanya idadi kubwa ya kuzidi nusu millioni ya watu waliozitembelea na kuona mambo na habari mbalimbali zinazohusu Zanzibar.
Kati ya watu hao duniani kote ambao kupitia katika links zetu hizo sio tu wameweza kufatilia soka la nchini bali wengi wao wameweza kufatilia ni nchi gani husika ambayo inazungumziwa na hivyo kuwafanya kati ya watu hao zaidi ya nusu millioni miongoni mwao kuvutiwa zaidi ya utalii hivyo kuweza kuvumbua Zanzibar kuwa ni sehemu kubwa na tulivu duniani kwaajili ya mapumziko ya holidays kwa watalii hao.
Pamoja na kwamba kituo chetu hakijanufaika hadi sasa na ujio huo wa watalii hapa nchini lakini kituo chetu kina kila sababu na kinazidi kujivunia manufaa yanayopatikanwa nchini kwa njia hio ya utalii zaidi ya kwa kituo chetu ni moja ya " chachu " ya maendeleo hayo katika sekta hio ya utalii.
Katika link ya plus.google.com idadi ya waliotembelea ni laki 444.467 wakati katika blog ya O.F.A idadi ikifikia 41,627 idadi hio kwa ujumla ni 486.094.
BAADHI YA PICHA NA IDADI YA WALIOZIANGALIA DUNIANI KOTE
Hizo ni baadhi ya picha zikiwa na idadi walioziangalia kupitia moja katika links zetu zinazomilikiwa na kituo chetu cha kukuza soka kwa vijana nchini cha Orange Football Academy.
idadi kamili kujumuisha na official website yetu pamoja na ile ya youtube itafuatia siku zijazo.