WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday, 25 July 2009

MABINGWA WA KNOCK-OUT ORANJE FOOTBALL ACADEMY ZIARANI MANGA PWANI KESHO

Vijana chipukizi wenye sifa ya kusakata soka ya kisasa Oranje Football Academy kesho watakuwa katika ziara ya siku moja katika mji wa Manga Pwani wilaya ya Kaskazini B,
wakiwa huko wataweza kutembelea sehemu mbali mbali za kitalii na kihistoria pamoja na kucheze mechi ya kirafiki na Timu ya soka ya Daraja la pili ya Aluta ya mji huo wa Manga Pwani,kutokana na timu hio ya Aluta kuwa timu ngumu na yenye wapenzi wengi katika mji huo tunatarajia mchezo wa kesho utakuwa na upinzani mkali na kutoa burudani safi kwa wapenzi wengi watakaofurika kuziona timu hizo mbili zikipambana kwa mara ya kwanza katika historia,hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa vijana wa Oranje football academy kufanya ziara kama hio ambapo itaweza kuwajenga vizuri chipukizi hao kisaikolojia,ambapo ziara njingi zitafatia ndani na nje ya nchi katika siku sijazo,kutokana na mipango mahiri inayofanywa na viongozi wao ni kuhakikisha chipukizi hao wanakuwa ni wawakilishi wazuri wa Taifa kwa kuwapeleka chipukizi hao katika vilabu mbali mbali nje kwaajili ya trials,na kujiunga na timu za huko kwa manufaa ya Taifa hapo baadae.
-------------------------------------------------------------------------------------------------

Wednesday, 22 July 2009

MABINGWA WA KNOCK-OUT,BONANZA CUP,NA WASHINDI WA TATU WA YOUTH U-17 KUFANYA ZIARA MANGA PWANI JUMAPILI

Mabingwa wa knock-out,bonanza cup,na washindi wa tatu wa ligi ya U-17 Oranje Football Academy jumapili ijayo tarehe 26-07-09 watakuwa ziarani katika mji wa Manga Pwani wilaya ya kaskazini B,
wakiwa huko wataweza kutembelea maeneo mbali mbali ya kihistoria pamoja na maeneo ya kitalii,
Wakaazi wa mji wa Manga Pwani na vitongoji vyake wataweza kupata burudani safi ya soka pale mabingwa hao Oranje football Academy watakaposhuka dimbani jioni hio kwa mchezo wa kirafiki na ALUTA timu ya daraja la pili ya mji huo wa Manga Pwani,
akiongea na mtandao huu wa O.F.A katibu mkuu ndugu Hussien alisema "Mpaka sasa mipango ya ziara hio inaendelea vizuri, na tunatarajia vijana wetu wataweza kupumzika vizuri kwa kuweza kubadilisha upepo wakiwa huko"
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Captain Nassir akiwa na kombe la ubingwa wa knock-out 2009.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
captain wa O.F.A akipokea zawadi ya jezi ambazo ni moja katika zawadi za ubingwa wa knock-out u-17 mwaka huu 2009.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
wachezaji wa O.F.A Yussuf(kushoto)na Miraji(kulia) wakiwa wamebeba kombe la mshindi wa tatu wa ligi ya youth U-17 mwaka huu 2009.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Naibu waziri kiongozi na waziri wa habari utamaduni na michezo mh Ali Juma Shamhuna (katikati mwenye kofia)akiwa katika picha ya pamoja na mabingwa wa Bonanza cup O.F.A mara baada ya kuwakabidhi kikombe pamoja na zawadi ya Tsh 200,000 baada ya kuitandika Shangani f.c kwa mabao 3-0 mwanzoni mwa mwaka huu 2009.
-------------------------------------------------------------------------------------------------

Monday, 20 July 2009

SEIF ABDALLA WA ORANJE FOOTBALL ACADEMY ACHAGULIWA KATIKA TIMU YA TAIFA YA VIJANA YA TANZANIA U-17 KUPITIA MKOA WA PWANI

Mshambuliaji hatari wa Oranje Football Academy Seif Abdalla ambae hivi sasa yupo kwa muda katika mji wa Bagamoyo amechaguliwa kuwa katika orodha ya mwanzo ya wachezaji wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania U-17 ambapo ametumia ticket ya mkoa wa pwani ambao aliuwakilisha katika mashindano ya copa coca cola yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita,
mshambuliaji huyo chipukizi mwenye uwezo wa hali ya juu wa kumiliki mipira,kasi na uwezo mkubwa wa kufunga mabao amekuwepo kwa muda mjini Bagamoyo kwa muda ambapo amekuwa akifanya mazoezi na Academy moja maarufu ya mijini hapo,
kutokana na uwezo wake mkubwa na kipaji cha soka alichonacho hakikuchukua muda kwa kijana huyo wa Oranje Football Academy kuonekanwa katika mkoa huo wa pwani na kumuita kuiwakilisha timu hio,ambapo aliweza kungára na kuonyesha uwezo wake wa hali ya juu hata kumfanya kocha wa timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania kutoka Brasil kumuona na kumuita katika kikosi chake alichokiteua katika hatua ya mwanzo
-------------------------------------------------------------------------------------------------

VIJANA WA ORANJE FOOTBALL ACADEMY YAWAADHIBU VIONGOZI WAO KWA MABAO 2-0

Katika mechi ya kusherekea kumalizika kwa michuano ya vijana mwaka huu 2009 ambapo O.F.A imeweza kupata matokeo mazuri kwa michuano hio kwa ujumla, leo ilipambana na viongozi wa cadaemy hio ambao ni wachezaji wa zamani waliopata kusifika wakati wao katika soka kwa kuwaadhibu jumla ya mabao 2-0 katika mchezo safi na wakuvutia wa kubadilishana mawazo,
katika mechi hio ilikuwa na kila aina ya ufundi vijana wa oranje football academy iliweza kuwafundisha walimu wao soka ya kitabuni na kuweza kutawala mchezo huo kwa muda mrefu,
hadi mwisho wa mchezo chipukizi hao wa O.F.A alitoka kifua mbele dhidi ya viongozi kwa magoli 2-0,
Wakati huo huo Mshambuliaji hatari wa chipukizi wa Oranje football academy Seif Abdalla ambae hivi karibuni amekuwa katika academy ya mkoa wa pwani kwa muda amechaguliwa kuwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania U-17 iliyochaguliwa mwishoni mwa wiki ambapo Seif amechaguliwa akitokea mkoa wa Pwani, Seif Abdalla ni mshambuliaji alieleta mafanikio mengi katika Academy na ni mchezaji ambae ni tegemeo katika academy ya O.F.A
------------------------------------------------------------------------------------------------

Sunday, 19 July 2009

ORANJE FOOTBALL ACADEMY YATOA PONGEZI KWA MABINGWA WA COPA COCA COLA

-------------------------------------------------------------------------------------------------
------------------------------------------------------------------------------------------------- Kwaniaba ya viongozi,wachezaji,na wapenzi wote wa ORANJE FOOTBALL ACADEMY wanatoa pongezi kwa timu ya mkoa ya mjini magharibi kwa kutwaa ubingwa wa copa coca cola kwa vijana wenye umri wa miaka 17, Oranje Football Academy ni moja ya timu za vijana ambao wanaiwakilisha mkoa huo wa mjini magharibi ambapo wachezaji wake wawili wapo katika kikosi hicho cha mabingwa hao wapya wa copa coca cola,
akiongea na mtandao unaomilikiwa na academy hio katibu mkuu wa O.F.A Hussien alisema" Academy ya O.F.A inawapongeza vijana hao kwa kutwaa ubingwa huo msimu huu na kuonyesha soka ya kuvutia ambapo vijana hao walionyesha vipaji vyao ambavyo ni hazina kubwa kwa taifa siku za baadae" aidha aliipongeza "timu ya mkoa wa Tabora kwa kuwa ni timu iliyoonyesha kiwango kizuri cha soka katika mashindano hayo",aliongeza kwa kuzipongeza timu zote za vijana zilizoshiriki katika mashindano hayo ambayo yameonyesha Tanzania kuwa na hazina kubwa ya vijana wenye vipaji nchini,na kupoteza kwa mikoa mingine kufikia fainali ni moja ya mchezo wa soka ambapo ni timu mbili tu ndizo zinahitajika kuingia fainali lakini kwa ujumla timu zote zilikuwa nzuri sana na vijana wanahitaji kutunzwa na kuendelezwa kwa juhudi zote kwa manufaa ya taifa hapo baadae, aliongeza katibu huyo kwa kusema" wakati umefika kwa makampuni mingine kuiga mfano wa kampuni ya coca cola kwa kuweza kuwasaidia vijana hapa nchini kwa lengo la kuipandisha nchi yetu katika ramani ya soka duniani"
-------------------------------------------------------------------------------------------------
COPA COCA COLA 2009 YAONYESHA TAIFA KUWA NA VIJANA NYOTA WA SOKA:
Michuano ya copa Coca cola ikiwa imemalizika na timu ya mjini magharibi ikiwa imetwaa ufalme mwaka huu 2009,ambapo vipaji mbali mbali vilijitokeza na kuonyesha uwezo wa hali ya juu kwenye michuano hio,kutokana na mashindano hayo Tanzania imefanikiwa kupata mwanga kwa wachezaji chipukizi wenye uwezo na ndio wenye nafasi ya kuunda kikosi cha timu ya taifa ya vijana ya Tanzania.
Timu ya mjini magharibi kutwaa ubingwa huo ilikuwa ni matarajio makubwa kutoka kwa wapenzi wote wa soka kulingana na kiwango cha hali ya juu kilichoonyeshwa na chipukizi hao kuanzia hatua ya makundi hadi ya mtoano,
ikiwa ni Timu pekee kutoka kisiwani Zanzibar iliyofanikiwa kuingia robo fainali ya michuano hio,ilifanikiwa kuzifunga karibu timu zote ilizokutana nazo na kufikisha idadi ya magoli 27.
Katika michuano hio Lindi ni timu pekee ambayo ilishindwa kuifunga au kutoka sare na timu zote ilizokutana nazo na kuondoka bila ya kuwa na pointi yoyote katika mchuano hio,
Timu zote zilionyesha kiwango kizuri katika mashindano hayo ambacho hakikutarajiwa na viongozi wa soka nchini pamoja na watazamaji wote kwa ujumla waliokuwa wakifatilia michuano hio,
pamoja na viwango vizuri ,vijana walionekana kuwa na maumbile makubwa yenye kuvutia ambayo ndiyo yanayotakiwa kwa wachezaji ambao hasa katika soka ya kulipwa kama wakiendelezwa vizuri na kutunzwa.
Hali ilijionyesha kuwa Tanzania ina hazina kubwa ya vijana wenye uwezo wa hali ya juu katika soka,sawa na mataifa mengine ,kama brasil,na west africa kama kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuwaweka chipukizi hao kama wanavyofanya wenzetu walioendelea kisoka,na hii itaweza kutoa nyota wengi kwenda kucheza soka ya kulipwa nje na kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zitakazotisha kisoka sio tu ukanda wa Africa bali duniani kwa ujumla.
Katika michuano hio jumla ya magoli 343 yalipachikwa wavuni na vijana hao tokea kuanza hadi kumalizika kwa michuano hio,kati ya magoli hayo vijana 7 walifanikiwa kupachika jumla ya magoli 3 kila mmoja kwa mchezo mmoja, hii ni moja ya kitu cha kujivunia kwa taifa kuwa na washambuliji vijana kama hao wenye uwezo na uchu wa kupachika mabao kimiani.
Mgeni rasmi wa kufunga michuano hio ya mwaka huu 2009 waziri wa habari,utamaduni na michezo George mkuchika aliiomba Serikali, Tff na kampuni hio ya coca cola kuongeza mkataba mwingine kwaajili ya kuendleza michuano hio kwa vijana ambao ni manufaa ya Taifa.
Nchi za Africa ya kusini,Zimbabwe,Msumbiji,Ethiopia,Kenya,Zambia,Uganda,na angola zimefaidika kwa kuuza wachezaji nje kutokana na michuano kama hio ambapo nchi kama brasil,argentine ikiwa ndio vinara wa kutoa wachezaji katika michuano kama hio kwa vijana wao kuonekanwa na vilabu mbali mbali, nyota wa zamani wa Argentine Diego Maradonna alianza kuingárisha nyota yake katika michuano kama hio ya coca cola cup na kumfikisha kuwa nyota ya dunia wakati wake.
Naye kocha wa mjini magharibi Juma Abdulrabi alisema"Kikosi hicho kimejengeka kulingana na juhudi ambazo zilionyeshwa na uongozi mzima wa mkoa huo hasa kwa kuwajali vijana kwa kuwapatia misaada mbalimbali kwaajili ya kukamilsha azma yao ya ubingwa na kilikaa kambini kwa muda wa miezi wiwili tu."
Michuano ya mwaka huu ya copa coca cola ilianza juni 28 na kumalizika fainali julai 18,ambapo Rais wa Jakaya Kikwete alihudhuria fainali hio alitaka vile vile michuano hio kuendelezwa kwaajili ya manufaa ya taifa hapo baadae.
Leo O.F.A wanacheza mechi ya kirafiki na viongozi wa O.f.A.
-------------------------------------------------------------------------------------------------

Thursday, 16 July 2009

ORANJE FOOTBALL ACADEMY KATIKA PICHA

O.F.A katika picha na moja ya makombe matatu waliyochukua mwaka huu 2009
-------------------------------------------------------------------------------------------------
ORANJE FOOTBALL ACADEMY wakiwa katika picha ya pamoja na kombe la mshindi wa 3 wa ligi ya U-17
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Captain Nissir Nassor akinyanyua kombe la ubingwa wa knock-out baada ya kushinda magoli mechi ya fainal kwa jumla ya magoli 2-1.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Captain Nassor Nassir Kulia na Mudrik Ali kushoto wakishikilia Kombe la mshindi wa tatu wa ligi ya youth u-17.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Wachezaji wa O.F.A yussuf Miraji Kushoto,na Yunus Abdalla kulia wakiwa na kombe
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Ismail Abeid kushoto,Muhene Majid kuliwa wakishikilia kombe la mshindi wa 3 youth U-17
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Makipa wa kutegemewa wa O.F.A mbele alieshikilia kombe Abdalla Sleiman,aliesimama Mohammed Sleiman wakiwa na kombe
-------------------------------------------------------------------------------------------------
mchezaji bora wa mashindano ya knock-out U-17 Mudathir Yahya akiwa na kikombe zawadi ya mchezaji bora knock-out 2009.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
"Man of The Match" Mudathir Yahya ambae pia ni mchezaji bora wa Knock-out youth U-17 akipokea zawaji ya uchezaji bora mara baada ya kumalizika mechi ya fainal ya knock-out ambapo O.F.A walitwaa ubingwa kwa kushinda magoli 2-1 dhidi ya F.C. Arizona.
-------------------------------------------------------------------------------------------------

Friday, 10 July 2009

PICHA ZA MATUKIO YA FAINAL KNOCK-OUT YOUTH U-17

MASHABIKI WA ORANJE FOOTBALL ACADEMY WAKIVAMIA UWANJA WA MAO TSE TUNG KWA FURAHA KUSHEREHEKEA UBINGWA WA KNOCK-OUT YOUTH U-17 AMBAO TIMU YAO YA O.F.A ILIIBAMIZA F.C ARIZONA KWA MABAO 2-1 NA KUIBUKA BINGWA KATIKA MECHI SAFI ILIYOWABURUDUDISHA WAPENZI WA SOKA WALIOKUWEPO UWANJANI KUSHUHUDIA FAINAL HIO.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
MASHABIKI WA O.F.A WA MARIKA MBALI MBALI WALISHINDWA KUJIZUWIA KUVAMIA UWANJA MARA BAADA YA KUMALIZIKA MECHI YA YA FAINAL KNOCK-OUT WIKI ILIYOPITA
-------------------------------------------------------------------------------------------------
MASHABIKI WA (ACADEMY YA O.F.A AMBAO WANASIFIKA KWA KUTANDAZA SOKA )WAKIWAVAMIA KWA FURAHA WACHEZAJI WAO NA KUWAKUMBATIA KWA KUWAPONGEZA MARA BAADA YA REFA KUMALIZA MCHEZO HUO WA FAINAL ILIYOFANYIKA WIKI ILIYOPITA AMBAPO O.F.A ILIIBUKA MSHINDI WA BAO 2-1.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
WACHEZAJI WA O.F.A WAKIWA KATKA PICHA YA PAMOJA NA KOMBE LA MSHINDI WA TATU WA LIGI YA YOUTH U-17
-------------------------------------------------------------------------------------------------
CAPTAIN NASIR WA ORANJE FOOTBALL ACADEMY AKINYANYIA KOMBE LA UBINGWA WA KNOCK-OUT YOUTH U-17 KATIKA MECHI ILIYOFANYIKA WIKI ILIYOPITA AMBAPO PIA ILIKUWA NI SIKU YA KUKABIDHI ZAWADI NA MAKOMBE KWA MADARAJA MBALI MBALI KWA TIMU ZA VIJANA,
ORANJE FOOTBALL ACADEMY NI MABINGWA WA KNOCK-OUT 2009.
-------------------------------------------------------------------------------------------------

Tuesday, 7 July 2009

PICHA ZA FAINAL KNOCK-OUT ORANJE FOOTBALL ACADEMY 2-1 F.C ARIZONA

kipa wa O.F.A Mohd Suleiman akipasha kabla ya mchezo wa fainali na fc arizona ambapo O.F.A waliibuka Bingwa kwa kushinda bao 2-1 mechi iliyofanyika katika kiwanja cha Mao Tse Tung.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
wachezaji wa O.F.A wakipasha misuli kabla ya mchezo wao wa Fainali na Fc Arizona
------------------------------------------------------------------------------------------------
wachezaji wa o f a wakisalimiana na wachezaji wa F C Arizona kabla ya mchezo wao wa fainali
O.F.A waliibuka na ushindi wa bao 2-1
------------------------------------------------------------------------------------------------
Captain wa F.C Arizona akimkagua khalifa(Ferdinand) suleiman wa O.F.A wakati wa mechi ya Fainal knock-out iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii.
-------------------------------------------------------------------------------------------------

Sunday, 5 July 2009

ORANJE FOOTBALL ACADEMY MABINGWA KNOCK-OUT 2009

Captain wa Oranje Football Academy Nassor Nasir akipokea zawadi jana katika kiwanja cha Mao Tse Tung mara baada ya mchezo wao wa fainal dhidi ya F.C Arizona ambapo O.F.A iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-1
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Wa kwanza kutoka kulia ni Ramadhan Madundo kocha wa O.F.A akifuatiwa na Hussein Ali katibu Mkuu wa O.F.A wakifuatilia kwa karibu mchezo wa fainali jana wakiwa jukwaa kuu jana
katika kiwanja cha Mao Tse Tung, Viongozi hao wawili wa O.F.A pia ni viongozi wanaosimamia kamati ya maalum inayosimamia mashindano yote ya vijana Zanzibar
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Mchezaji wa Oranje Football Aademy Muhene Majid akifuatiwa na mmoja wa kiongozi wa O.F. A kupokea zawadi zao baada ya kushinda mchezo wao Fainali ya knock-out jana katika kiwanja cha Mao Tse Tung.
------------------------------------------------------------------------------------------------

Saturday, 4 July 2009

ORANJE FOOTBALL ACADEMY YATWAA TAJI JINGINE LA YOUTH KNOCK-OUT U17

Mabingwa wapya wa Knock-out 2009 kwa timu za youth U-17 wamepatikana dakika chache zilizopita,Oranje Football Academy vijana wenye kusakata soka la kisasa wameweza kutwaa ubingwa leo katika kiwanja cha mao tse tung kwa kuichapa timu ya vijana ya F.C Arizona kwa jumla ya mabao 2-1,

katika mchezo safi ambao ulimalizika dakika chache zilizopita mechi ambao ilikuwa kali na upinzani mkubwa kwa pande zote mbili,

katika mechi hio ya leo ya Fainal mabao ya vijana machachari wa O.F.A yalifungwa moja kwa kila kipindi, bao la kwanza lilifungwa na mshambulia hatari Said Mbaroud(malouda)

na lile la ushindi lilipachikwa wavuni na Yahya Mudathir katika kipindi cha pili,

kwa ushindi wa leo O.F.A itakuwa imetwaa mataji mawili msimu huu 2009 baada ya kutwaa ubingwa wa Bonanza Cup mwanzo mwa mwaka huu,
katika mechi ya leo O.F.A wamewakosa washambuliaji wao wawili Seif Abdalla(kahire) pamoja na Ali Hilali(Lee) ambao wapo katika mashindano ya Coca Cola Cup yanayondelea jijini Dar es Salaam,
pamoja na wachezaji hao imewakosa wachezaji wake kadhaa ambao wanasumbuliwa na maumivu mbali mbali waliyoyapata wakati wa mazoezi kujiandaa na mechi hio ya leo,
pamoja na kuwapoteza wachezaji hao muhimu vijana hao wa O.F.A wamekuwa na hazina kubwa ya chipukizi wenye vipaji vikubwa na ndio iliyopelekea leo kuweza kuendeleza kutembeza kichapo kwa kila timu wanayokutana nayo na kutwaa ubingwa kwa mara nyingine kwa mwaka huu 2009,
picha na maelezo zaidi kupatikana baadae katika blog hii inayomilikiwa na chipukizi hao wa Oranje Football Academy.

Friday, 3 July 2009

DEN HEIJER KUKUTANA NA VIONGOZI PAMOJA NA WACHEZAJI WA ORANJE FOOTBALL ACADEMY

Mwandisho na mpangaji wa shughuli mbali mbali za kituo cha kukuza soka kwa vijana nchini O.F.A Isabel Den Heijer kutoka The Netherlands atakutana na viongozi wote pamoja na wachezaji wa O.F.A hivi karibuni katika tarehe ambayo itatolewa hapo baadae ya kufika kwake,

katika mambo mbali mbali ya kukuza soka kwa kituo hicho cha O.F.A ataweza kuwaona vijana hao pamoja na kuwa na mazungumzo na viongozi wote wa kituo hicho kwalengo la kupata ripoti mbali mbali na kubadilishana mawazo na malengo ambayo yatafatia katika siku za hivi karibuni,

moja ya malengo ambayo atayazungumzia ni kuweza kurejea Holland na ripoti nzuri ambazo ataweza kuanza kipango ya kukifanya kituo hicho kuwa na ushirikiano mkubwa na wakaribu kutoka Holland,ambapo lengo nikuifanya Holland kuwa ni kituo kikubwa cha majaribio pamoja na kuchezea vilabu mbali mbali vya hapo,

mbali na Holland pia Den Heijer ataweza kuandaa mipango rasmi ya kuiunganisha Belfast- Nothern Ireland kuwa pia ni moja ya vituo vya chipukizi hao wa O.F.A cha kupeleka wachezaji hao,

ataweza kuzungumzia pia kuhusu ushiriki wa O.F.A wa YOUTH MILK TOURNAMENT ambapo itafanyika mji wa Belfast-Nothern Ireland nakuzishirikisha timu mbali mbali za bara la ulaya pamoja na south america,

Den Heijer hivi sasa tayari wiki hii amewasili Nairobi-Kenya ambapo yupo kikazi,anatarajiwa kuwasili nchini mara baada ya kumaliza shughuli zake za kikazi ambapo atakuwepo nchini Kenya kwa muda miezi miwili kabla ya kuja nchini ambapo atakuwepo kwa muda wa wiki 2 hadi 3.

ORANJE FOOTBALL ACADEMY KUJITUPA KATIKA FAINAL YA KNOCK-OUT KESHO IKIWA NA UPUNGUFU MKUBWA WA NYOTA WAKE

Oranje Football Academy Kesho watajitupa kiwanja kwa ajili ya mchezo wa fainali na f c arizona akiongea na blog ya O.F..A katibu mkuu wa Huessein Ali alisema "mchezo wetu wa kesho utakuwa ni mgumu sana kwavile tutacheza tukiwa na upungufu ya wachezaji wetu wawili ambao wote wamo katika kikosi cha kwanza yaani 11, hii inatokana na vijana hao kuwemo katika mashindano ya copa coca cola ambayo yanafanyika dar es salaam kitaifa"

aliendelea kwa kusema "vijana hao wawili watakaokosekana kwa mchezo wa kesho wa fainali ni seif abdalla rashid (karihe) striker na ali hilal (lee) defender vijana hawa wanaweza kuisababishia timu kuwa na mchezo mgumu zaidi kwani kocha ampaka jana usiku alikua na matumaini makubwa ya kuwapata vijana hawa hasa kwa vile hivi sasa timu ina majeruhi katika nafasi za washambuliaji na viungo"

alimalizia kwa kusema "hata hivyo timu inategemea kuonesha kandanda safi na kushinda mchezo huo,mchezo huo unatarajiwa kufanyika saa 8 kamili za mchana katika kiwanja cha mao tse tung.

Wednesday, 1 July 2009

TANZANIA YAPANDA KIWANGO CHA SOKA DUNIANI HADI NAFASI YA 97 BAADA YA KUIFUNGA "ALL WHITES" MWEZI ULIOPITA

Tanzania imepanda kiwango cha soka duniani kutoka nafasi ya 109 hadi kufikia nafasi ya 97,
hii ni habari njema kwa Taifa katika mwezi huu wa 07-2009,Tanzania imeweza kupanda ngazi 12 juu yake kutoka katika nafasi iliyokuwepo kabla ya tarehe 03-06-09 nafasi ya 109, hii inatokana na kushinda mechi ya mwisho ya kirafiki kati yake na New Zealand kwa mabao 2-1 katika kiwanja cha taifa-dar es salaam, kutokana na ushindi huo hivi sasa Tanzania itakuwa na kiwango bora cha soka duniani zaidi kuliko New Zealand yenyewe ambao hivi sasa wapo katika nafasi ya 100 duniani kwa mujibu wa Fifa world Ranking iliyotoka leo, hii itapelekea furaha kubwa kwa Watanzania pamoja na kocha Maximo,kabla ya mechi ya stars /New Zaland, "all Whites" walikuwa wana kiwango bora ukilinganisha na stars,kutokana na kiwango cha Tanzania kupanda hii inaonyesha kuwa Tanzania inahitajia mechi nyingi za kirafiki na timu zenye kiwango kizuri duniani kwani inapelekea kuipandisha rank kubwa ya kisoka duniani pindipo Stars wakishinda mechi hizo,
kwamaana hio Tanzania itakua inashika nafasi ya 3 kwa soka kwa nchi za Africa mashariki na Kati ikitanguliwa na Uganda nafasi ya 75,sudan 91,Tanzania 97,mabingwa wa CHAN 2009 D.R. Congo wanashika nafasi ya 102,Ethiopia 138,Kenya pamoja na kuwa wanashriki katika world cup qualification wanashika nafasi ya 105,malawi 110,Rwanda ambao kiwango chao cha soka kwa miaka mingi kilikuwa ni bora kuliko Tanzania wanashika nafasi ya 113,Washiriki wa Fainali za kombe la dunia zilizopita 2006 zilizofanyika ujerumani -Angola wanashika nafasi ya 103,
kuna mlolongo wa timu za Europer ambazo Tanzania inakiwango kikubwa cha soka duniani kama vile Georgia 104,Luxamburg 119,Montnegro 98, hii inaonyesha Kiwango cha Tanzania kimepanda sana kutokana na kuwafungwa mabingwa wa Oceania "All Whites" mwezi uliopita na inatakiwa Tanzania ijiamini kuweza kuagizia na kwenda kucheza mechi na timu kubwa kwa nchi za bara la ulaya ili kuweza kuipandisha kiwango zaidi nchi pamoja na kuweza kuwatanga wachezaji wetu nje,tunatarajia pia kutokana na ligi kuu Tanzania kutawaliwa na wachezaji wa kigeni itapelekea kuongeza viwango vya soka nchini na tunatarajia katika miaka michache inayofata Tanzania itakuwa ni nchi ya pili kwa ligi bora kwa nchi za Africa mashariki na kati pamoja na kusini mwa Africa baada ya south Africa ambapo wachezaji wengi wa Africa wamekuwa wakikimbilia huko kwa miaka mingi kwenda kucheza soka,
Hongera Taifa stars, Honger Watanzania kwa ujumla.
------------------------------------------------------------------------------------------------
-------------------------------------------------------------------------------------------------
------------------------------------------------------------------------------------------------
-------------------------------------------------------------------------------------------------

ORANJE FOOTBALL ACADEMY KUINGIA KAMBINI LEO

Oranje football academy wanaingia kambili rasmi leo kwaajili ya kujiandaa na pambano la fainal ya knock-out youth U-17 ambayo itafanyika tarehe 04-07-09 kati yake na A.C. Arizona,
katibu mkuu wa O.F.A Ali Hussein ametangaza kuwa wachezaji wote wako katika hali nzuri na wataingia kambini leo kwaajili ya mechi hio ambayo itakuwa ni ya upinzani mkubwa, aliongeza katibu huyo kuwa wapo katika hali nzuri ya kushinda na kutwaa ubingwa huo ambapo ameahidi kuonyesha kandanda safi kutokana na vijana wake kuwa na vipaji vikubwa katika soka.
-------------------------------------------------------------------------------------------------